Mwezeshaji
kutoka Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Dk.Emmarold Mneney
(kulia), akitoa mafunzo ya siku moja ya kilimo kwa wakulima wa Mkoa wa
Lindi kwenye Maonyesho ya Kitaifa ya Nanenane yanayoendelea kwenye
viwanja vya Ngongo mkoani hapa jana. Mafunzo hayo yaliandaliwa na Tume
ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)
Wakulima wakiwa kwenye mafunzo hayo
Utambulisho ukifanyika.
Ofisa Kilimo na Umwagiliaji wa Wilaya ya Kilwa, John Ignas Mkinga, akifungua mafunzo hayo.
Wakulima wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Mkulima Jakazi Ali kutoka Kilwa akielezea masoko ya kuuza mazao yao yalivyo na changamoto.
Mkulima Rashid Hassan kutoka Lindi vijijini akielezea jinsi konokono wanavyoathiri mazao yao.
Mkulima Saada Makota kutoka Wilaya ya Nachingwea akichangia jambo kwenye mafunzo hayo.
Betty Milanzi mkulima kutoka Wilaya ya Nachingwea akielezea changamoto za kilimo wanazokumbana nazo.
Mkulima Mwanajumbe Nchuwa kutoka Kilwa akichangia jambo kwenye mafunzo hayo.
Mratibu
wa Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB), Dk. Philbert
Nyinondi ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo Morogoro (SUA),
akiwaeleza wakulima hao umuhimu wa kutumia simu zao kupata masoko ya
mazao yao na kuwasiliana na wakulima wenzao katika masuala ya kilimo.
…………………………………………………………………
Na Dotto Mwaibale, Lindi
WAKULIMA
wa Mkoa wa Lindi wameiomba serikali kuchukua hatua za haraka ili
kudhibiti konokono ambao wametajwa kuwa ni tishio kwa uharibifu wa mazao
ya chakula na biashara mkoani humo.
Ombi
hilo walilitoa katika mafunzo ya siku moja ya kilimo yaliyotolewa na
Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) katika maonyesho ya
kitaifa ya wakulima Nanenane yanayoendelea viwanja vya Ngongo mkoani
hapa jana.
“Tunachangamoto
nyingi katika kilimo lakini kubwa zaidi ni konokono ambao wapo katika
mashamba yetu ambao wanashambulia mimea ikiwa michanga na hata tukiwaua
wamekuwa wakiongezeka jambo ambalo linatukatisha tamaa” alisema Rashid
Hassan mkulima kutoka wilaya ya Lindi vijijini.
Alisema
hawajui konokono hao wanatoka wapi na wafanyeje ili kumaliza changamoto
hiyo ambayo imekuwa ni kilio kikubwa kwa wakulima wa mkoa huo kwani
konokono hao wamekuwa wakila majani ya mmea ambayo ni machanga.
Mkulima
Saada Makota kutoka Wilaya ya Nachingwea alisema changamoto waliyo nayo
kucheleweshewa kufika kwa pembejeo za kilimo kwa wakati na ugonjwa wa
kutu unaoshambulia mikorosho na kuifanya ikauke majani yake kwa juu.
“Pembejeo
za kilimo tunaletewa mwezi wa tatu wakati mvua zimeanza kunyesha badala
ya mwezi wa Desemba jambo ili linaturudisha nyuma wakulima” alisema
Makota.
Mwanajumbe
Nchuwa mkulima kutoka Kijiji cha Luato wilayani Kilwa alilamikia bei ya
ufuta kushushwa na walanguzi kutoka sh.2000 kwa kilo hadi 1500 kwa
mtindo wa choma choma.
Mkulima
Betty Milanzi kutoka Kijiji cha Nammanga Nachingwea alisema changamoto
nyingine waliyonayo ni wanyama waharibifu wa mazao yao kama nyati,
tembo, nguruwe hivyo wakaomba serikali kupitia idara ya wanyapori
iwasaidia kumaliza changamoto hiyo.
Mwezeshaji
wa mafunzo hayo kutoka Jukwaa la Bioteknolojia kwa maendeleo ya Kilimo
(OFAB), Dk. Hamalord Mneney aliwataka wakulima hao kubadilika na kulima
kilimo chenye tija na kufuata maelekezo ya wataalamu badala ya kuendelea
na kilimo ambacho hakina manufaa kwao.
Alisema
lengo la mafunzo hayo ni kubadilishana uzoefu na kuona ni jinsi gani
sayansi na teknolojia inavyoweza kutumika katika kilimo cha kisasa
katika mazao yote ya chakula na biashara yanayolimwa katika mkoa huo.
Mkulima
Saada Makota aliomba muda wa mafunzo hayo uongezwe ili waweze kupata
fursa zaidi ya kujifunza na kupeleka elimu hiyo kwa wakulima waliowengi
katika maeneo yao.
Mratibu
wa Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB), Dk.Philbert
Nyinondi ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo Morogoro (SUA),
aliwataka wakulima hao kutumia simu zao kutafuta masoko ya mazao yao na
kupeana taarifa mbalimbali ili kukabiliana na changamoto wanazo
kabiliana nazo katika kilimo.
SHARE
No comments:
Post a Comment