Viongozi
wakuu wa Afrika Kusini wamekubali mechi wa kufuzu kwa kombe la dunia
mwaka 2018 ambapo Afrika Kusini iliibuka mshindi inastahili kurudiwa.
Shirikisho la kandanda duniani
FIFA lilitoa ilani kwamba mechi hiyo irudiwe baada ya mwamuzi wa mechi
hiyo Joseph Lamptey kupigwa marufuku kwa kutoisimamia vyema mechi hiyo.
Shirikisho la kandanda wa Afrika
Kusini (Safa) limekuwa likitathmini jinsi ya kukata rufaa lakini kwa
sasa wamesema wamekubaliana na Fifa hata hivyo shirikisho hilo limesema
lingekata rufaa iwapo mashtaka ya mwamuzi huyo yngebatilishwa.
Afrika Kusini iliichapa Senegal
magoli 2-1 katika mechi waliotoka sare mwaka jana na Siku ya Jumanne
Safa ilisema ”imeamua kwa misingi ya kimaadili na nidhamu kwamba mechi
hii ilibatilishwe.
”Iwapo korti itabatilisha uamuzi
huo, kila kitu kitakuwa hakitambuliki na Safa watakosa nafasi ya kukosoa
uamuzi wa Fifa wa kurudia mechi hiyo.
”Maelezo yote ya Safa kwamba kazi zake hazihusiani na hongo, basi kwa misingi hiyo ndio tumeamua kuyafuata maagizo ya Fifa.”
Safa imekuwa ikifikiria kukata rufaa kwani ilikuwa imeshauriana na wachunguzi ambao walikuwa wakifanyia mechi hiyo uchunguzi.
Hii inamaanisha Afrika Kusini sasa
wako katika nafasi ya mwisho katika kundi D na alama moja katika mechi
tatu walizoshiriki na sasa Senegal wako katika nafasi ya tatu na alama
nne.
Burkina Faso imeongoza katika
kundi lake na alama sita , mbele ya taifa la kisiwani Cape Verde
kutokana na tofauti ya goli moja, huku ikiwa na mshindi katika hatua ya
makundi ndiye atakaye fuzu katika michuano ya kombe la Dunia itakayo
andaliwa nchini Urusi.
Fifa itatoa uamuzi wake tarehe 14
kwa siku halisi kwa mechi hiyo ya marudiano , ambayo inatarajiwa
kuchezwa katika dirisha la uhamisho wa kimataifa- mwezi mmoja kabla droo
ya Kombe la Dunia mwaka 2018.
Afrika kusini wala Senegal hazijalaumiwa kwa makosa yoyote.
SHARE
No comments:
Post a Comment