Afisa Mtendaji wa Zuku Fiber, Mhandisi Thomos Hintze akizungumza na
waandishi katika uzinduzi wa Internet Fiber iliyofanyika jana jijini Dar
es Salaam, Kulia ni Meneja wa Zuku Fiber Thomas Wenanga pamoja na Mkuu
wa kitengo cha Fiber, Michael Debaly
Meneja Uendashaji wa Zuku Fiber, Mcharo Mlaki akizungumza katika
uzinduzi wa huduma ya Internet iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Zuku Fiber, Mhandisi Thomos Hintze akiwa na watendaji wa kampuni hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Kampuni ya Zuku imezindua huduma ya Internet yenye uwezo mkubwa wa kuweza kufanya kazi kwa vitu vitatu kwa wakati mmoja.
Akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam jana, Afisa Mtendaji wa Zuku Fiber, Thomos Hintze
amesema kuwa Zuku Fiber inawezo mkubwa kuliko mitandao mengine iliyopo
nchini.
Amesema kuwa wamejipanga kutokana
na kampuni hiyo kuwa na miundombinu inayojitosheleza ambapo mtu akilipia
anapata huduma muda huo huo
Hata hivyo amesema kifurushi cha
Zuku fiber triple Play 100 mbps kimeundwa ili kukidhi mahitaji ya
mtandaoni kama video fupi, sinema , michezo ya kuigiza na video za
mawasiliano.
Hintz amesema kuwa gharama za mtandao huo ni sh .79,000 ambapo Mteja anapoanza kutumia uwezo wake ni uleule mpaka mwisho.
Amesema kampuni hiyo imekwenda mbali baadhi ya nchi za Afrika ambazo ni Zambia, Malawi, Uganda pamoja na Kenya
SHARE
No comments:
Post a Comment