Diamond Platnumz atakuwa mwanafamilia mpya kwenye kuitangaza bidhaa hiyo na kuungana na Mastaa kibao duniani ambao pia ni mabalozi wa bidhaa hiyo akiwemo Rick Ross. Baada ya taarifa hizo rapa kutoka Marekani Rick Ross, nae pia alimkaribisha Diamond Platnumz kupitia ukurasa wake wa
Instagram kwa kuandika ‘Self Made Tastes Better’
caption iliyoambana na picha ya Diamond Platnumz . Dili hilo ambalo bado
halijawekwa wazi ni kiasi gani Diamond Platnumz ataingiza baada ya
kusaini na kampuni hiyo, lakini huenda likawa ni dili la mamilioni ya
fedha kwani Rick Ross ambaye pia ni Balozi wa Belaire anakadiriwa
kulipwa kiasi cha Dola milioni 4.1, zaidi ya Tsh bilioni 8.
SHARE








No comments:
Post a Comment