Usiku wa September 14 2017 michezo wa UEFA Europa League hatua ya
Makundi msimu wa 2017/2018 ilichezwa barani Ulaya kwa michezo zaidi ya
nane kuchezwa katika viwanja mbalimbali, zaidi ya miaka 20 usiku wa
September 14 2017 tumeishuhudia club ya Arsenal ikicheza kwa mara ya
kwanza michuano hiyo ya Europabaada ya miaka 20.
Arsenal ambao walikuwa katika dimba lao la nyumbani la Emirates
dhidi ya Koln FC ya Ujerumani walifanikiwa kuondoka na ushindi wa
magoli 3-1, licha ya kuwa wamekuwa hawafanyi vizuri katika michezo yao
ya Ligi Kuu England msimu wa 2017/2018 na kuambulia kushinda mechi 2
kati ya mechi 4 walizocheza hadi sasa na wapo nafasi ya 11.
Licha ya kuwa mchezo ulichelewa kuanza kwa sababu ya
mashabiki kuleta fujo kidogo, Koln ndio walikuwa wa kwanza kupata goli
dakika ya 9 kupitia kwa Jhon Cordoba na magoli ya Arsena yalifungwa na
Sead Kolasinacdakika ya 49, Alex Sanchez dakika ya 67 na Hector Bellerin
dakika ya 82 Matokeo ya game za Europa League msimu wa 2017/2018
zilizochezwa Alhamisi September 14 2017
No comments:
Post a Comment