Dereva huyo akiwa amelazwa hospitali baada ya kujeruhiwa.
DEREVA wa Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini, John Heche (Chadema)
amevamiwa na watu wasiojulikana kisha kumkata kwa mapanga usiku wa
kuamkia leo majira ya saa 2 usiku huku ikielezwa kuwa hali yake si
nzuri. Ndugu na marafiki wakimjulia hali hospitalini hapo. Taarifa hizo za kusikitisha zimethibitioshwa na Bosi wa Dereva huyo
ambaye ni Mbunge John Heche kupitia Katibu wake,Mrimi Zablon ambaye
amekiri kuwa dereva huyo anayefahamika kwa jina la Suez Daniel maradufu
ni kweli amepata shambulio hilo na sasa yupo hospitali akipatiwa
matibabu. Mbunge, John Heche.
TAARIFA KWA UMMA Jana majira ya saa mbili usiku dereva
wa mbunge John Heche anayejulikana kwa jina la SUEZ DANIEL MARADUFU
alivamiwa na watu wasiojulikana na kushambuliwa kwa kukatwa katwa na
mapanga kichwani na hali yake si nzuri, anaendelea na matibabu kwenye
Hospitali ya Bomani Tarime. Ofisi ya Mbunge Jimbo la Tarime Vijijini
15/9/2019.
No comments:
Post a Comment