Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto
amemtaka dereva wa Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema)Tundu Lissu,
ajitokeze ili aweze kutoa maelezo yake kuhusiana na tukio la kupigwa
risasi bosi wake. Kamanda huyo amesema kwamba sababu ya kumtafuta dereva
huyo aliyemtaja kwa jina la Adam ni kwa sababu alikuwa pamoja na
majeruhi wakati tukio hilo linatokea.Pia Kamanda huyo alimtaka Katibu Mkuu wa Chadema Dk Vicent Mashinji kufika kwa RCO mjini Dar es Salaam ama Dodoma kutokana kauli yake kuwa katika uchunguzi wao wamewabaini wahusika. Kamanda Muroto amesema Polisi Mkoani Dodoma wamekamata magari nane aina ya Nissan Patrol kwa ajili ya uchunguzi wa tukio la kupigwa kwa risasi kwa mbunge wa Singida Mashariki (Chadema)Tundu Lissu.
Kamanda Muroto amesema uchunguzi huo unafanywa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA). “Uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa wahalifu walikuwa na silaha ya SMG/SAR kutokana na maganda ya risasi yaliyokutwa eneo,” pia amesema Polisi Dodoma limekamata magari 8 aina ya Nissan Patrol kwa ajili ya uchunguzi wa tukio la kupigwa kwa risasi Tundu Lissu, RPC Muroto asema
SHARE








No comments:
Post a Comment