Askofu Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima amefunguka na
kusema kuwa siku ya Jumapili atafanya maombezi maalum kwa afya ya Mbunge
Tundu Lissu ambaye juzi alipigwa risasi na watu wasiojulikana akiwa
Dodoma nyumbani kwake.
Askofu Gwajima amesema kuwa atatumia misa hiyo kulaani vikali kitendo
cha kinyama alichofanyiwa Tundu Lissu na watu hao wasiojulikana ambao
waliweza kupiga gari lake zaidi ya risasi 30 huku risasi tano ndizo
ziliweza kumjeruhi Mbunge huyo.
"Jumapili hii Septemba 10, 2017 nitaongoza maombi maalumu ya kuombea
Afya ya Mhe. Tundu Lissu na kulaani Vikali kitendo cha Kikatili na
Kinyama alichofanyiwa. Maombi haya yatafanyika katika Kanisa la Ufufuo
na Uzima, Ubungo Dar es Salaam tunawakaribisha wote watakaopenda
kuungana nasi katika maombi haya" aliandika mchungaji Gwajima kupitia
ukurasa wake wa facebook
SHARE
No comments:
Post a Comment