Kampuni ya Panasoniki ya Japan
imetoa taa za sola pamoja na chaji zake 600 zilizopokelewa na Wakala
wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa niaba ya Serikali kupitia Shirika
la Maendeleo Duniani -UNDP kwa ajili ya wakazi wanaoizunguka Misitu
asilia 12 ya hifadhi inayomilikiwa serikali kuu.
Akikaribisha ugeni huo Msaidizi wa
shirika la Kimataifa la UNDP, Amon Manyama , amesema shirika lao
linalenga kuondoa umaskini, Afya Bora na usawa wa Kijinsia , hivyo zoezi
hili linalenga kupunguza Umaskini kwa wananchi wanaozunguka Misitu ya
hifadhi na kujenga dhana ya ushirikiano katIka kuhifadhi Misitu hiyo.
Mratibu wa mradi wa Hifadhi wa
Misitu asilia hiyo, Gerald Kamwenda amesema Misitu hiyo asilia kila
moja ina asili ndwele ambayo inapatikana katika msitu huo tu. Amesema
Msitu wa amani ambao ndiyo mkongwe na wa kwanza kuhifadhiwa una amfibia
aina 3, ndege aina 3, reptilia aina 2 na uufugaji wa vipepeo,
Amezitaja hifadhi nyingine kuwa ni
Rondo, Mkingu,Nilo,Chome,Magamba, Uluguru, kilombero, Mlima Rungwe,
Mlima Hanang, Minziro na Udzungwa ambazo pia zina aina tofauti ya asili
zinazovutia.
Kamwenda amesema taa hizo za sola zitaimarisha uhusiano na wakazi wanaozunguka Misitu asilia iliyohifadhiwa.
Naye balozi wa Japan nchini,
Masaharu Yoshida amesema anafurahi kwa sababu nchi yake inaimarisha
ushirikiano na nchi ya Tanzania kwa kupitia watanzania wahitaji na
watunza mazingira kwa kuwapatia vifaa vya kiteknolojia vinavyorahisisha
dhana ya maendeleo ya uchumi kwa jamiijambo ambalo pia linaimarisha
ushirikiano wa Kampuni binafsi na serikali.
Akikabidhi Taa hizo Rais wa
Panasonic Tanzania Bwana Katshiko Mori amesema Shirika lake linasimamia
kaulimbiu inayosema Maisha bora, Dunia bora kwa hiyo wanayo furaha
kuyabadilisha maisha ya wakazi wanayozunguka Misitu iliyohifadhiwa ,
wanaamini wanabadili maisha yao kuwa bora kwa kuwapatia bidhaa zenye
ubora wa juu kwa gharama nafuu.
Akipokea msaada huo kwa niaba ya
serikali mtendaji Mkuu wa wakala wa Huduma za misitu Profesa dos santos
silayo amesema Changamoto inayotukabili mpaka sasa ni nishati ya gharama
nafuu ili kupunguza matumizi ya Nishati ya mkaa ambapo mpaka sasa
nishati inayotumika mi asilimia 90 inatoka katika Mimea.
Msaada huu ni Muhimu kwa sababu
inawaongezea uwezo wakazi wenye kipato kidogo kutumia nishati rahisi na
endelevu ya moto jambo linalopeleka kupunguza matumizi ya nishati
itokanayo na Mimea na hivyo kulinda Mazingira na Misitu kwa ujumla.
SHARE
No comments:
Post a Comment