KIKAO cha Kamati Maalum ya
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, kinatarajiwa kufanyika kesho Septemba 18
mwaka huu, chini ya Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar
Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein.
Taarifa kwa vyombo vya habari
iliyotolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar wa Idara ya
Itikadi na Uenezi Mhe. Waride Bakari Jabu, imesema kikao hicho cha siku
moja kitafanyika katika Ukumbi wa Afisi kuu ya CCM, Kisiwandui kuanzia
saa 4:00 asubuhi.
Pamoja na mambo mengine, kikao
hicho kitapokea na kujadili kwa kina taarifa ya Hali ya Kisiasa ya
Zanzibar pamoja na taarifa nyengine mbali mbali kutoka Idara na Vitengo
vya Chama Cha Mapinduzi Zanzibar, vile vile kikao hicho kitapokea na
kujadili majina ya wana CCM waliojitokeza kuomba kuteuliwa kugombea
nafasi ya Mwenyekiti wa CCM katika ngazi za Wilaya kwa kipindi cha
2017-2022, kwa upande wa Zanzibar na kutoa mapendekezo yake kwa
Halmashauri Kuu ya Taifa.
Kikao hicho kilitanguliwa na
kikao cha Sekretarieti ya Kamati Maalum ya NEC – Zanzibar kilichofanyika
Septemba 16, mwaka huu, chini ya Mwenyekiti wake Naibu Katibu Mkuu wa
CCM Zanzibar, Dk.Abdulla Juma Saadalla “Mabodi”, kwa ajili ya kuandaa
Ajenda za kikao hicho.
SHARE
No comments:
Post a Comment