Na Unique Maringo
MAHAKAMA ya Hakimu
Mkazi Kisutu imehairisha kesi ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin
inayomkabili mfanyabiashara Yusufu Manji.
Wakili wa utetezi
Hajra Mungula mbele Hakimu Mfawidhi Cyprian Mkeha alieza kuwa kesi hiyo
imekuja kwaajili ya kusikilizwa na wako tayari.
Alidai kuwa mteja
wake anahitaji kutoka kwa ajili ya matibabu kwasababu yuko nje kwa
dhamana, aliomba mahakama kesi hiyo iweze kusikilizwa siku tatu
mfululizo.
Kwa upande wake Wakili wa serikali Timon Vitalis alidai kuwa anataka kusafiri mchana na hatoweza kusikiliza kesi hiyo.
Hakimu Mkeha alisema
kuwa anakwenda kwenye kikao na kuahirisha shauri hilo ambalo
litasikilizwa siku tatu mfululizo kwanzia Septemba 25 hadi 27.
Inadaiwa kuwa,kati ya Februari 6 na 9, 2017 katika eneo la Upanga Sea View Ilala alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin.
Kesi hiyo ipo katika
hatua za usikilizwaji wa mashahidi upande wa utetezi ambapo shahidi wa
kwanza katika kesi hiyo, Mkugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya
Kikwete (JKCI) Prof.Mohamed Janabi aliieleza mahakama kuwa Manji ana
Vyuma kwenye moyo.
Baada ya kesi hiyo
kuahirishwa nje ya Mahakama Manji alisalimiana na mashabiki wa klabu ya
Yanga waliokua mahakamani hapo pamoja na mchezaji wa timu hiyo Nadr
Haroub maalufu kwa jina la Canavaro.
Mbali na Canavaro pia
benchi la ufundi la Yanga likiongozwa na kocha George Lwandamina nao
walihudhuria mahakamani hapo katika kesi inayomkabili aliyekua
mwenyekiti wa klabu ya Yanga.
SHARE
No comments:
Post a Comment