KESI inayowakabili Rais wa Klabu
ya Simba, Evans Aveva na Makamu wake, Godfrey Nyange maarufu kama Kaburu
upelelezi wake umekamilika na jalada lao limefikishwa kwa Mkurugenzi wa
Mashtaka nchini (DPP) kwa ajili ya kupitiwa ili kuona kama ushahidi unajitosheleza.
Kesi hiyo
iliyotajwa leo Mahakamani Kisutu, mbele ya Hakimu Victoria Nongwa,
imeahirishwa hadi Septemba 27 mwaka huu itakaposikilizwa.
Aveva na Kaburu wanashtakiwa
na TAKUKURU wakikabiliwa na tuhuma za kughushi nyaraka za Klabu ya Simba
na kutakatisha fedha kiasi cha dola za Marekani 300,000 (zaidi ya Sh
milioni 650) na wamekuwa rumande tangu Juni 29, mwaka huu.
Upelelezi uliokuwa unafanyiwa kazi
ni nyaraka za kughushi maandiko zilizokuwa zimepelekwa kwa mtaalam
kufanyiwa uchunguzi ili kubaini makosa hayo.
SHARE
No comments:
Post a Comment