Msanii Sharifa Salum Hassan wa Kikundi
cha Tausi kutoka Kisiwandui akionyesha umahiri wa kucheza ngoma kwenye wa Ufunguzi wa
Tamasha la Wasanii Wanawake wa mkoa wa Kusini Unguja lililofanyika
kwenye ukumbi wa Coco Blue, Jambiani ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. (
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Wasanii wa Kikundi cha Majalis Saniya kutoka Michenzani wakitumbuiza
wakati wa Ufunguzi wa Tamasha la Wasanii Wanawake wa mkoa wa Kusini
Unguja lililofanyika kwenye ukumbi wa Coco Blue, Jambiani ambapo mgeni
rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan. ( Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akiangalia baadhi ya vitu vilivyotengenezwa na mikono wakati wa
Ufunguzi wa Tamasha la Wasanii Wanawake wa mkoa wa Kusini Unguja
lililofanyika kwenye ukumbi wa Coco Blue, Jambiani jana jioni. (Picha na
Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan jana alifungua Tamasha la Wasanii Wanawake wa mkoa wa
Kusini Unguja.
Tamasha hilo lililofanyika kwenye ukumbi wa Coco Blue
,Jambiani na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali wa Chama na Serikali
pamoja na wananchi wa mkoa wa Kusini Unguja.
Makamu wa Rais aliwashukuru Waandaaji wa Tamasha hilo
ambao wamesaidia kuwaleta wanawake wa mkoa wa Kusini pamoja.
Makamu wa Rais amewapongeza wanawake wa mkoa wa Kusini
kwa kuwa wa kwanza kutekeleza wazo lililowazwa na kuonyesha utamaduni wa
Kusini.
Mhe. Samia alisema Utamaduni wa zamani hauna budi
kuendelezwa ili vijana wa sasa wajue wapi tumetoka, wapi tulipo na wapi
tunaelekea.
Akivitaja baadhi ya vitu alivyoviona kwenye ufunguzi
huo kama Manda, Mabobwe ,Vipopoo, ngoma ya Msanja ambavyo kwa pamoja vina lengo
la kuleta yale mazuri ya zamani ambayo yametutoka.
Alisema Vijana wengi hawajui Kiwe-jiwe la kusagia
chakula (Blender za Bibi zetu) wao wanajua Blender, hivyo ni vyema
Tamasha hili likaja na vitu vingi mwakani waelewe hata maji tuliyatunza kwenye
Mtungi ambao wao kwa sasa wanayajua Majokofu.
Hivyo aliwasihi Wanawake wa kusini kufufua tamaduni
zetu na kuzidumisha, alisema sema yeye anatoka Kizimkazi ambapo ngoma
maarufu ni Shomoo na Dandaro .
Makamu wa Rais alisema kuwa Utamaduni utasaidia
kuwafunza watoto wetu uzalendo,mazingira, nidhamu ya maisha kwani
utamaduni unajumuisha kila kitu kuanzia chakula, mavazi, vifaa
vilivyotumika,filamu, ngoma na burudani mbali mbali.
Mhe. Samia aliwapongeza sana wanawake wa mkoa wa
Kusini kwa kutoka kwenye utamaduni wa kukaa tu na badala yake kufanya shughuli
zinazowaingizia kipato. “Nimefurahishwa
kuona wakina Mama sasa hivi wanatoka wana Vikundi vya Kulima tumeonyeshwa
wanalima Tungulee, wanalima Karoti,wanalima michicha hii yote ni utamaduni
kwamba tumetoka kwenye utamaduni wa kukaa tu na kusubiri bwana haji lakini sasa
tunatoka tunajituma na sisi tunapata mapato yetu tunaendelea na maisha yetu”
Makamu wa Rais alisema ni wajibu wa kila mama kutunza
na kufundisha watoto wetu Tamaduni zetu, “Tunautamaduni ambao hautakiwi kuonyeshwa mbele za watu na ule nao
tufundishe watoto wetu, tusiuache , tunakuwa wa kisasa mno , tunajifanya wa
kisasa mno kiasi ambacho mambo mengine tunayaacha lakini ambao kwa sie
tuliofanyiwa huko nyuma unajua faida yake na watoto wetu wanaokosa kufanyiwa
sasa hivi tunaona hasara yake”
Mwisho Makamu wa Rais alitoa rai kwa waandaaji wa
Tamasha hilo kuhakikisha linafanyika kila mwaka na kujumuisha tamaduni mbali
mbali zenye lengo la kujenga na kuimarisha mshikamano pamoja na kudumisha
upendo na amani katika jamii, aliwashukuru wadhamini waliosaidia
kufanikisha Tamasha hilo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akiangalia baadhi ya vitu vilivyotengenezwa na mikono wakati wa
Ufunguzi wa Tamasha la Wasanii Wanawake wa mkoa wa Kusini Unguja
lililofanyika kwenye ukumbi wa Coco Blue, Jambiani jana jioni. (Picha na
Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akiangalia baadhi ya vitu vilivyotengenezwa na mikono wakati wa
Ufunguzi wa Tamasha la Wasanii Wanawake wa mkoa wa Kusini Unguja
lililofanyika kwenye ukumbi wa Coco Blue, Jambiani jana jioni. (Picha na
Ofisi ya Makamu wa Rais)
Wasanii wa Kikundi
cha Tausi kutoka Kisiwandui wakitumbuiza wakati wa Ufunguzi wa
Tamasha la Wasanii Wanawake wa mkoa wa Kusini Unguja lililofanyika
kwenye ukumbi wa Coco Blue, Jambiani ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. (
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
SHARE
No comments:
Post a Comment