Balozi wa Marekani
kwenye Umoja wa Mataifa ameilaumu Korea ya Kaskazini kwa kulazimisha
vita kutokana na majaribio yake ya makombora ya mara kwa mara.
"Vita sio kitu ambacho Marekani ingetaka," alisema. "Hatutaki vita kwa sasa lakini uvumilivu wa nchi yetu hautuzuii."
- Korea Kaskazini inajiandaa kufanya majaribio zaidi ya makombora
- Bomu la Korea Kaskazini: Tunayoyajua kufikia sasa
Hata hivyo, China imesisitiza wito wake wa kutaka pande zote zirudi katika meza ya mazungumzo.
Ripoti zinasema kuwa Korea Kaskazini inajiandaa kwa majiribio mengie ya makombora.
Haley amesema teknolojia ya Korea ya Kaskazini kwenye mabomu ya nyukilia ni ya hatari na haina mfano
Siku ya Jumapili ilifanya jaribio la bomu la chini ya ardhi lililoaminika kuwa na nguvu ya kati ya kilotani 20 na 120.
Kifaa hicho hicho kinaweza kuwa na nguvu mara tatu zaidi ya bomu lililotumiwa kuharibu mji wa Hiroshima mwaka 1945.
China haitaki kuwepo nchi yenye silaha za nyuklia ya Korea Kaskazini na mara kwa mara imeeleza msimamo wake kwa nchi hiyo.
Lakini pia haitaki kuona utawala wa Korea Kaskazini ukiondolewa madarakani. Hii itasababisha mamilioni ya wakimbizi kukimbia kwenda China na kuchangia kuungana kwa Korea ambayo itakuwa chini ya ushawishi wa Marekani.
CHANZO: BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment