
Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za
Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Ephraim Kwesigabo akizungumza
na waandishi wa habari jana Dar es Salaam wakati akitoa taarifa ya
Mfumuko wa Bei wa mwezi Agosti, 2017 ambao umepungua hadi kufikia
asilimia 5.0 ikilinganishwa na asilimia 5.2 ilivyokuwa mwezi Julai,
2017.

Baadhi ya Waandishi wa Habari
wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Ephraim Kwesigabo wakati akitoa taarifa
ya Mfumuko wa Bei wa mwezi Agosti, 2017 ambao umepungua hadi kufikia
asilimia 5.0 ikilinganishwa na asilimia 5.2 ilivyokuwa mwezi Julai,
2017.
………………………………………………………….
Na: Veronica Kazimoto-Dar es Salaam
Mfumuko
wa Bei wa Taifa kwa mwezi Agosti, 2017 umepungua hadi kufikia asilimia
5.0 ikilinganishwa na asilimia 5.2 ilivyokuwa mwezi Julai, 2017. Hii
inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa
mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2017 imepungua ikilinganishwa na mwezi
Julai, 2017.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Sensa na
Takwimu za Jamii Ephraim Kwesigabo wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu amesema
kupungua kwa Mfumuko wa Bei wa mwezi Agosti, 2017 kumechangiwa na
kupungua kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula.
Kwa
upande wa thamani ya shilingi ya Tanzania, Kwesigabo amesema uwezo wa
Shilingi 100 katika kununua bidhaa na huduma umefikia Shilingi 92 na
senti 20 mwezi Agosti 2017 ikilinganishwa na Shilingi 91 na senti 87
ilivyokuwa mwezi Julai, 2017.
Mfumuko
wa Bei ambao hupima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na
huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi, una mwelekeo unaofanana na
nchi ya Uganda ambapo Mfumuko wa Bei umepungua hadi asilimia 5. 20
mwezi Agosti, 2017 kutoka asilimia 5.70 mwezi Julai, 2017. Nchini Kenya,
Mfumuko wa Bei wa mwezi Agosti, 2017 umeongezeka hadi asilimia 8.04
kutoka asilimia 7.47 mwezi Julai, 2017.
SHARE








No comments:
Post a Comment