
USAJILI WA WAZEE WA WILAYA YA UBUNGO VITAMBULISHO VYA TAIFA
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
(NIDA), inapenda kuwajulisha wazee wote wa mkoa wa Dar-es-salaam Wilaya
ya Ubungo kuwa, zoezi la Usajili na Utambuzi lenye lengo la kuwapatia
Vitambulisho vya Taifa linaendelea sambamba na zoezi la Usajili wa Kadi
za Bima ya Afya kwa wazee chini ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.
Wahusika ni wazee wote wanaoishi
Wilaya ya Ubungo. Unachotakiwa kufanya ni kuchukua na kujaza fomu ya
maombi ya Usajili. Fomu zinapatikana ofisi ya Mtaa unakoishi au Ofisi
ya Kata. Unapojaza fomu ya maombi unatakiwa kuweka na nakala ya
viambatisho muhimu vinavyokutambulisha vile ulivyonavyo mathalani Kadi
ya Kupigia kura, Barua ya Serikali ya Mtaa, vyeti vya shule na kisha
fika na fomu yako ikiwa imejazwa pamoja na vivuli (photocopy) ya
viambatisho hivyo kwenye kituo cha karibu kusajiliwa.
Unapofika kusajiliwa unashauriwa
kwa ajili ya ubora wa picha kutovaa nguo nyeupe, kijivu, bluu, pinki, au
rangi yoyote inayoshabihiana na nyeupe, nguo zenye nembo, kofia aina
yeyote ama kupaka hina kwenye viganja vya mikononi.
Kwa kuanza wiki ijayo Ratiba ya Usajili itakuwa ni kama ifuatavyo:-
| Na | KITUO CHA USAJILI | MUDA | TAREHE |
| 1. | Kata ya Makurumla | Saa 3:00 – 11:00 jioni | 11/09/2017 |
| 2. | Kata ya Manzese | Saa 3:00 – 11:00 jioni | 12/09/2017 |
| 3. | Kata ya Sinza | Saa 3:00 – 11:00 jioni | 13/09/2017 |
| 4. | Kata ya Makuburi | Saa 3:00 – 11:00 jioni | 14/09/2017 |
Utaratibu wa Usajili katika Kata zingine tutaendelea kuwafahamisha. Kupata maelezo zaidi tafadhali wasiliana na mtendaji wako wa Mtaa au Mtendaji Kata.
Kwa taarifa zaidi kuhusu
Vitambulisho vya Taifa tembelea Tovuti yetu www.nida.go.tz au ukurasa
wetu wa facebook -nidatanzania au twitter @nidatanzania
Wazee jitokezeni kusajiliwa Vitambulisho vya Taifa ili mtambulike na kupata huduma za kijamii kwa haraka na kwa uhakika zaidi.
Limetolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)
SHARE








No comments:
Post a Comment