Rais wa Zimbabwe
Robert Mugabe ameagiza usajili mpya wa wapiga kura wakati nchi hiyo
inajitayarisha kwa uchaguzi mkuu mwaka ujao.
Rais Robert Mugabe
Zimbabwe itafanya uchaguzi mkuu mwaka ujao kwa kutumia dafatri hiyo mpya ya usajili wa wapiga kura , ikiwa ni mojawapo tu ya mageuzi ya uchaguzi yalioitishwa na upinzani kwa muda mrefu
.
Agizo hilo la rais linasema usajili unapaswa kuanza September 14 hadi Januari mwaka ujao. Mfumo huu mpya unaidhinishwa kwa kutumia vifaa vilivyonunuliwa hivi karibuni kutoka China.
Usajili utajumuisha kunakiliwa alama za vidole na ithibati ya ukaazi. Dafatari hilo la usajili limekumbwa na mzozo katika uchaguzi wa siku za nyuma Zimbabwe.
Mnamo 2008 vyama vya upinzani vilisema waligundua makosa ikiwemo kusajiliwa kwa wapiga kura wengi waliokuwa wanasemekana kuishi katika eneo moja, na wengine katika maenoe yasioishi watu.
CHANZO: BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment