
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akitoa salaamu za pole za
Serikali na Wizara yake jana Jijini Dar es Salaam wakati wa kuaga mwili
wa Mkuu wa Wilaya mstaafu na Mwanahabari Marehemu Muhingo Rweyemamu
aliyefariki Septemba 2 mwaka huu katika hospitali ya Agha Khan.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akitoa heshima za mwisho jana Jijini Dar es Salaam kwa mwili wa Mkuu wa Wilaya mstaafu na
Mwanahabari Marehemu Muhingo Rweyemamu aliyefariki Septemba 2 mwaka huu
katika hospitali ya Agha Khan.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe.
Paul Makonda akitoa heshima za mwisho jana Jijini Dar es Salaam kwa
mwili wa Mkuu wa Wilaya mstaafu na Mwanahabari Marehemu Muhingo
Rweyemamu aliefariki Septemba 2 mwaka huu katika hospitali ya Agha
Khan.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bibi
Sophia Mjema akitoa heshima za mwisho jana Jijini Dar es Salaam kwa
mwili wa Mkuu wa Wilaya mstaafu na Mwanahabari Marehemu Muhingo
Rweyemamu aliefariki Septemba 2 mwaka huu katika hospitali ya Agha
Khan.

Mkuu wa Wilaya ya Handeni
Bw.Godwin Gondwe akizungumza wakati wa kuaga mwili wa mkuu wa wilaya
mstaafu na Mwanahabari Marehemu Muhingo Rweyemamu aliefariki Septemba 2
mwaka huu katika hospitali ya Agha Khan.

Mtoto wa marehemu Muhingo
Rweyemamu Bw. Emmanuel Muhingo akisoma wasifu wa baba yake aliefariki
Septemba 2 mwaka huu katika hospitali ya Agha Khan wakati wa kuagwa jana
Jijini Dar es Salaam .

Baadhi ya waombolezaji
wakifuatilia tukio la kuaga mwili wa Mkuu wa Wilaya mstaafu na
Mwanahabari Marehemu Muhingo Rweyemamu aliyefariki Septemba 2 mwaka huu
katika hospitali ya Agha Khan.
…………………..
Na Shamimu Nyaki-WHUSM
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo Mhe Dkt. Harrison Mwakyembe ameongoza mamia ya waombolezaji
kuaga mwili wa Mkuu wa Wilaya mstaafu na Mwanahabari, marehemu Muhingo
Rweyemamu aliyefariki Septemba 2 mwaka huu katika hospitali ya Agha
Khan.
Akitoa salamu za pole kwa niaba ya
Serikali na Wizara yake jana Jijini Dar es Salaam, Mhe. Mwakyembe
amemuelezea marehemu Rweyemamu kuwa alikua mtumishi mzuri katika
Serikali hasa katika wadhifa wake wa Ukuu wa Wilaya na mara zote
alihakikisha Wananchi anaowaongoza wanakuwa wachapakazi kwa maendeleo
yao na Taifa kwa ujumla.
“Serikali inatoa pole sana kwa
familia na wanatasnia ya habari kwani marehemu Rweyemamu ameacha pengo
kubwa kwa familia yake na wanahabari kutokana na uhodari wake katika
uandishi lakini pia Serikali inakumbuka uchapakazi wake alipokua
Serikalini. Tunaomba Mungu awape faraja na uvumilivu wafiwa wote”.
Alisema Mhe. Mwakyembe.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya
Handeni Mhe. Godwin Gondwe amemuelezea marehemu kuwa alikuwa mchapakazi
hodari wakati alipokuwa Mkuu wa Wilaya hiyo na Wananchi wa Handeni
watamkumbuka katika jitihada zake za kuhimiza watoto wa kike kupenda
shule ambapo alianzisha kampeni iliyoitwa “niache nisome” lengo likiwa
ni kuelimisha umuhimu wa elimu kwa mtoto wa kike.
“Wananchi wa handeni
wamesikitishwa sana na kifo hiki kwani wanakumbuka uhodari wake katika
kuwatumikia alipokuwa mkuu wa Wilaya yao hasa juhudi zake za kuhimiza
jamii kupeleka watoto shule kwa manufaa yao ya baadae”. Alisema Mhe.
Gondwe”.
Naye mwakilishi kutoka vyombo vya
habari Bw. Absolum Kibanda amesema kuwa marehemu alikuwa mwalimu na
mshauri mzuri katika tasnia ya habari na alikuwa anaipenda kazi yake na
kufanya waandishi wengi kuiga na kujifunza kutoka kwake uandishi wa
habari za uchunguzi na makala.
Marehemu Muhigo Ryeyemamu amewahi
kufanya kazi katika magazeti ya mbalimbali hapa nchini ikiwemo
Mtanzania, Mwananchi, Rai, The Citizen akitumikia nyadhifa mbalimbali
kama mhariri na mwandishi. Marehemu amezikwa leo katika makaburi ya
Kinondoni Jijini Dar es Salaam na ameacha mke,watoto wanne na mjukuu
mmoja
SHARE
No comments:
Post a Comment