Na Binagi Media Group.
Utafiti
mpya uliofanywa na Taasisi ya Taifa Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu
nchini (NIMR) umebaini kwamba magonjwa ya Malaria, Ukimwi, Moyo, Mfumo
wa Upumuaji pamoja na Upungufu wa Damu yanayongoza kwa kusababisha vifo
vya hospitalini.
Aidha
utafiti huo ambao uliofanyika mwaka jana kwa kutumia takwimu za kuanzia
mwaka 2006 hadi 2015 katika hospitali 39 nchini ambazo ni pamoja na
hospitali ya Taifa, hospitali za Kanda, Hospitali za mikoa na wilaya
umeonyesha kwamba vifo vya ajali vimeongezeka kwa asilimia 16, saratani
asilimia 24, kiharusi asilimia 27 na kisukari asilimia 11.
Akizungumza
kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mwanza hii leo Jijini Mwanza kwenye
uwasilishaji wa matokeo ya utafiti huo katika mikoa ya Kanda ya Ziwa
pamoja na Kanda ya Magharibi, Mganga Mkuu mkoani Mwanza Dkt.Leonard Subi
amesema hatua madhubuti zinapaswa kuchukuliwa kwa kutumia utafiti huo
ili kudhibiti vifo hivyo.
Mtafiti
Mkuu Kiongozi kutoka NIMR, Dkt.Leonard Mboera amesema utafiti huo pia
ulilenga kuangalia upatikanaji wa takwimu za vifo katika hospitali
nchini Tanzania ambapo ilibainika kuwepo changamoto katika ukusanyaji,
uchanganuzi na matumizi ya takwimu katika hospitali.
Taasisi
ya NIMR ilifanya utafiti ili kubaini sababu na vyanzo vya vifo katika
hospitali nchini Tanzania na kubaini kwamba ugonjwa wa Malaria unaongoza
kwa kusababisha vifo kwa asilimia 12.8, Mfumo wa upumuaji kwa asilimia
10.1, Ukimwi asilimia 8.0, upungufu wa damu asilimia 7.8, magonjwa ya
moyo na mfumo wa damu asilimia 6.3 huku mikoa ya Dar es salaam, Mwanza
na Morogoro ikiongoza kwa vifo katika hospitali nchini.
Mgeni
rasmi, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dkt.Leonard Subi akizungumza
kwenye warsha hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John
Mongella. Warsha hiyo imejumuisha washiriki kutoka mikoa ya Kigoma,
Kagera, Geita, Tabora, Shinyanga, Mara, Simiyu na Mwanza.
Dkt.Changalucha John ambaye ni Mkurugenzi Mkuu NIMR kituo cha Mwanza akizungumza kwenye warsha hiyo
Mtafiti Mkuu Kiongozi kutoka NIMR, Dkt.Leonard Mboera, akizumza na wanahabari nje ya warsha hiyo
Dkt.Omari Gamuya akitoa neno la shukurani kwa niaba ya Mganga Mkuu mkoani Mara
Mmoja wa watafiti kutoka NIMR akifafanua jambo mbele ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kuhusu utafiti huo
Washiriki wa warsha hiyo
Baadhi ya washiriki
Mgeni
rasmi, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt.Leonard Subi (wa tatu waliokaa)
akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi pamoja na washiriki mbalimbali
wa warsha hiyo.
Picha ya pamoja
SHARE
No comments:
Post a Comment