TRA

TRA

Wednesday, September 13, 2017

PIKIPIKI 356 ZAKAMATWA TANGA

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


ZAIDI ya Pikipiki  350 alimaarufu bodaboda zimekamatwa na Jeshi laPolisi Mkoani Tanga kutokana na makosa  mbalimbali ya usalama barabarani ikiwemo madereva wake kutokuvaa kofia ngumu pindi watumiaji vyombo hivyo.



Pikipiki hizo zilikamatwa wakati wa operesheni ya Jeshi hiloinayoendelea katika maeneo mbalimbali Jijini Tanga  ikiwa ni mkakati wa kupambana uvunjifu wa sheria za usalama barabarani na kupunguza ajali
ambavyo vimekuwa zikigharimu maisha ya wananchi.

Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga Benedict Wakulyamba (Pichani Juu} aliwaambia waandishi wa habari kuwa zoezi la ukamati wa pikipiki hizo limetokana na ukaidi wa madereva na abiria wa kutokutii sheria za barabarani ikiwa pamoja kutokuwa na leseni .

Alisema katika ukamataji huo pikipiki 206 ambazo zilikamatwa na madereva wake wakikabiliwa na makosa ya kutokuwa na kofia ngumu, madereva 87 hawakuwa na leseni,pikipiki 33 hazikuwa na bima 25 mbovu na 5 kuzidisha abiria(mshikaki).

Aidha alisema kufuatia hali hiyo jeshi hilo baada ya kujiridhisha na hatua za kisheria pikipiki 244 zilitozwa tozo za papo kwa pao,32 dereva na abiria wake walifikishwa mahakamani,32 walionywa kutokana na
utaratibu wa kisheria na 48 bado zipo kituo cha polisi cha mabawa kwa hatua zaidi za kisheria.

“Niseme tu kutii sheria bila shuruti limeonekana kama jambo geni hasa hapa Jijini kwetu na watu walifikiri ni kitu hakiwezekani lakini tumeliamua kweli na tutashughulika nao wanaokaidi sheria za barabarani”Alisema Kamanda Wakulyamba.

Alisema kumekuwepo na malalamiko dhidi ya jeshi hilo kuwa ukamataji wa pikipiki hizo hauzingatii utaratibu wa kisheria kutokana na namna ya ukamataji wake unavyofanyika ikiwa pamoja na askari kuvaa kiraia na
hata kuwavizia katika baadhi ya maeneo.

“Hatuwezi kupangiwa jinsi ya kumkamata mtu tunayemuhisi anamakosa,kinachofanywa na askari wangu ni kumsimamisha mwendesha boadaboda au chombo chochote cha moto lakini kama hataki kutii tunalazimika kumkamata kwa njia yoyote”Alisema Wakulyamba.

Hata hivyo amewatahadharisha wananchi Mkoani hapa kuwa zoezi hilo si nguvu ya soda na litaendelea ikiwa sehemu ya kukomesha virendo vya kutokutii sheria za barabarani na hakutakuwa na simile kwa atakae
kamatwa awe derva au abiria wote wataingia kwenye makosa.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger