TRA

TRA

Friday, September 15, 2017

PPRA NA NEEC ZAINGIIA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO WA MIAKA MITANO

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA Dkt.  Laurent  Shirima, (kulia), akibadilishana hati na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i  Issa, baada ya kusaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili utakaodumu kwa miaka mitanmo. Mkataba huo mumesainiwa jijini Dar es Salaam Septemba 14, 2017. (PICHA NA EMMANUEL MASAKA WA BLOGU YA JAMII)

MAMLAKA ya  Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) na  Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), wametiliana saini mkataba wa miaka mitano wa ushirikiano
Mkataba huo uliosainiwa leo Septemba 14, 2017 jijini Dar es Salaam, utawezesha PPRA na NEEC kushirikiana   kiutendaji  ili kuwawezesha  wajasiriamali wadogo  na wa kati   kushiriki   kwenye fursa   mbalimbali  zinazopatikana katika manunuzi ya umma.
Akizungumza wakati wa hafla ya utilianaji saini  mkataba huo,  Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA Dk.  Laurent  Shirima, lengo linguine ni mamlaka  kuhakikisha  kigezo mojawapo  wakati wa  hatua ya tathimini kwenye zabuni za umma  cha  upendeleo kwa ajasiriamali  wadogo na kati kinazigatiwa.
“Pia  kila mwaka PPRA na NEEC kufanya tathimini ya pamoja ili  kujua namna taasisi nunuzi  zinavyotekeleza au kuzingatia ushiriki wa wajasiriamali wadogo na wakati,”alisema Dk. Shirima.
Malengo mengine ni PPRA na NEEC kufanya tafiti za pamoja  zitakazo jikita  zaidi  katika uwezeshaji  na ushiriki wa wajasiriamali  wadogo na kati  kwenye michakato ya  manunuzi  ya umma.
“Suala la kuwajengea wananchi uwezo  wa kupambana na umasikini kwa kushiriki katika shughuli za kiuchumi limekuwa  kipaumbele kikubwa  cha serikali na hasa ya awamu ya tano.
Ili kufanikisha azma hiyo , serikali imekuwa ikiandaa sera  na sheria  mbalimbali  zinazoweka mazingira  mazuri  ya wananchi  kushiriki na kuitumia fursa za kibiashara,”lifafanua Dk. Shirima.
Alisema  moja ya sekta  inayotoa  fursa kwa wananchi  kushiriki kwenye shughuli za kukuza uchumi wan chi ni sekta ya manunuzi  ya umma, hivyo  wananchi mmojammoja au kwa makundi  wakijengewa uwezo wanaweza kuchangamkia  fursa  zilizopo  kwenye sekta hiyo  ikiwa ni pamoja na kushuriki  kwenye  hatua mbalimbali ya zabuni zinazotolewa na taasisi za umma.
“Ni matuani yetu kwamba wananchi  walio katika  makundi  husika watachangamkia fursa  hii  ya kujwakwamua kiuchumi na kijamii katika maeneo yao,”alibainisha.
Alisema taasisi za ununuzi, hasa halmshauri  zinatarajiwa  kutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa sheria ili kufanikisha lengo la serikali  la  kutoa upendelea kwa makundi  maalum  yamekuwa yanashindwa kunufaika na fursa zilizo katika sekta ya ununuzi wa umma.
Kwa upande wa  Katibu Mtendaji wa NEEC, Beng’I Issa, alisema  kupitia  ushirikiano huo watahakikisha  tathimini ya ushiriki  wa biashara ndogo na za kati  unafanyika katika  ukaguzi  wa ununuzi wa taasisi za umma.
“Pia taasisi ambazo zitatoa zabuni  kwa wafanyabiashara wadogo  na wakati kwa kiwango  kilichoainishwa  katika  sheria  kwa makundi maalum ya wanawake, vijana na watu wenye  ulemavu kutambuliwa,”alisema Beng’i.
Alisema utekelezaji wa ushirikiano huo  unalenga kuhakikisha  biashara, kampuni au vikundi  vinavyomilikiwa  hasa  na wanawake , vijana na watu  wenyeulemavu zinapata fursa  kushiriki  kwenye zabuni za taasisi za umma.
“Hii itasaidia  kukuza uchumi  wao ili kutekeleza ibara ya 57(e)(vi) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Pia kuwezesha  kutathimini  ushiriki  wa biashara ndogo na za kati ili kupata takwimu sahihi zitakazowezesha  serikali  kuchukua hatua stahiki za kuwawezesha,”alibainisha.



Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA Dkt.  Laurent  Shirima,(kulia), pamoja na Katibu Mtendaji wa NEEC, Beng’i Issa wakisaini mkataba wa miaka mitano wa ushirikiano wanaoshuhudia  (kulia )ni  Mwanasheria Mwandamizi wa PPRA, Agnes Sayi  na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Ushiriki wa Watanzania katika Uwekezaji, Esther Mmbaga.



Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA Dkt.  Laurent  Shirima, (kulia), akizugumza wakati  wa hafla ya utilianaji saini wa mkataba wa miaka mitano wa ushirikiano baina ya PPRA na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC)  Septemba 14, 2017 jijini Dar es Salaam.(kushoto) ni Katibu Mtendaji wa NEEC, Bi. Beng’i  Issa

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger