Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza
kushoto), akikagua jenereta linalowezesha mnara wa Kampuni ya Simu
Tanzania (TTCL), katika eneo la eneo la Gairo Hill,wilayani Gairo,
Mkoani Morogoro. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Bibi.
Siriel Mchembe.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia),
akijadiliana jambo na Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Bibi. Siriel Mchembe,
kabla ya kuzungumza na wananchi wa kata ya Leshata, wilayani Gairo,
Mkoani Morogoro.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza
kushoto), akimsikiliza Mtendaji mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote
(UCSAF), Mhandisi Peter Ulanga (kulia) alipokagua minara ya simu
wilayani Gairo, Mkoani Morogoro.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza
kushoto), akitoa maelekezo kwa Wafanyakazi wa Kampuni ya Vodacom
Tanzania mara baada ya kufungua mnara wao katika kijiji cha Chakwale
wilayani Gairo, Mkoani Morogoro.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameyataka
makampuni ya simu nchini kuhakikisha mawasiliano ya simu yanapatikana
wakati wote katika ubora unaotakiwa ili kuwawezesha wananchi kupata
huduma inayowiana na thamani ya fedha wanayolipa.
Akikagua
na kuzindua minara ya simu ya kampuni za TTCL, VODACOM, HALOTEL, na
TIGO katika Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro, Profesa Mbarawa amesema
Serikali itaendelea kushirikiana na kampuni za simu kupitia Mfuko wa
Mawasiliano kwa wote UCSAF ili katika kipindi cha miaka mitatu ijayo
sehemu zote za Tanzania ziwe zimefikiwa na huduma ya mawasiliano ya simu
ya uhakika.
“Tumieni
mawasiliano ya simu kufanya biashara, kuboresha huduma za jamii kama
elimu na habari ili kukuza ustawi wa maisha yenu”, amesema Profesa
Mbarawa.Waziri
Prof. Mbarawa amewaonya wananchi kujiepusha na matumizi mabaya ya
mitandao ya simu kwani ipo sheria kali inayodhibiti matumizi mabaya ya
simu.
Amezungumzia
umuhimu wa kampuni za simu kujenga minara katika maeneo mapya na
kukarabati minara ya zamani ili kuwezesha mawasiliano kuwa katika ubora
maeneo yote ya nchi.Amewataka
wakazi wa vijiji vya Letugunya, Leshata na Chakwale kutumia fursa ya
upatikanaji wa mawasiliano kuongeza uzalishaji wa mazao na kuyauza kwa
bei nzuri na hivyo kukuza uchumi wao.
Kwa
upande wake Mtendaji mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote Mhandisi
Peter Ulanga amemhakikishia Waziri Profesa Mbarawa kuwa mfuko huo
umejipanga kukamilisha miradi yote kwa wakati na kufanya uhakiki wa
takwimu za mawasiliano nchi nzima ili kubaini maeneo ambayo yana
changamoto kubwa ya mawasiliano na kuyatatua.
Mkuu
wa Wilaya ya Gairo Siriel Mchembe amemshukuru Waziri Mbarawa kwa
kuboresha huduma za mawasiliano katika Wilaya hiyo na kumhakikishia
wananchi watailinda miundombinu hiyo ili idumu kwa muda mrefu.
SHARE
No comments:
Post a Comment