RAIS John Magufuli ameivunja Mamlaka ya Usimamizi wa Mji Mdogo wa
Kigamboni (KDA) na sasa shughuli zake zinahamishiwa katika Manispaa ya
Kigamboni.
Akizungumza leo Jumatano Septemba 13, 2017,Waziri wa Ardhi,Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema ametumwa na Rais Magufuli kutangaza
uamuzi huo.
"Kumekuwa na mgongano katika usimamizi wa ardhi kati ya KDA na
Manispaa ya Kigamboni, Rais ameliona hilo na kuamua kuivunja mamlaka
hiyo,"amesema.
Lukuvi amesema jukumu la KDA lilikuwa kusimamia upangaji wa mji wa
Kigamboni wakati hilo pia ni jukumu la manispaa hiyo.
Lukuvi ametoa miezi sita kwa watendaji wa KDA kukamilisha makabidhiano ya
nyaraka na wao kuripoti kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni.
Mapema Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa amesema mgongano wa
usimamizi wa ardhi Kigamboni ulisababisha migogoro mingi ya ardhi.
Amesema pia manispaa hiyo ina upungufu wa maofisa mipango miji.
Amesema manispaa ina maofisa mipango miji watatu badala ya saba
wanaohitajika.
SHARE
No comments:
Post a Comment