Jumapili ya September 10, 2017 muamuzi wa kike wa
mchezo wa mpira wa miguu Bibiana Steinhaus ameandika rekodi mpya barani
Ulaya kwa kuwa muamuzi wa kwanza wa kike kuwahi kuchezesha mechi ya Ligi
Kuu Ujerumani Bundesliga.
Bibiana Steinhaus mwenye umri wa miaka 38 ameweka rekodi ya kuwa
muamuzi wa kwanza wa kike katika Ligi tano kubwa barani Ulaya
(Ufaransa, Hispanai, England, Ujerumani na Italia) kuwahi kuchezesha
mechi za Ligi Kuu za wanaume.
Mchezo wa Hertha Berlin dhidi ya Werder Bremen wa
Bundesliga uliyochezwa leo na kumalizika kwa sare ya 1-1, ulichezeshwa
na Bibiana Steinhaus ambaye nje ya urefa ni askari Polisi, mchezo wa leo
ndio mkubwa wa wanaume aliyowahi kuuchezesha. Bibiana ameanza kazi ya uamuzi toka mwaka 2007 hadi kufikia hapo
amechezesha michezo zaidi ya 80 ya Ligi daraja la pili, amechezesha
fainali ya wanawake ya Champions League 2017 na michuano ya wanawake
yaOlympic 2012 London lakini tegemea kuendelea kumuona Bundesliga wa
2017/2018 akichezesha mechi kadhaa.
No comments:
Post a Comment