Na Mathias Canal, Dar es salaam
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A.
Mwalimu Septemba 4, 2017 amezindua Ugawaji wa vitambulisho vya awali
7296 vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya
Ubungo Jijini Dar es salaam.
Akizungumza
katika uzinduzi huo uliofanyika katika Viwanja vya TP Sinza E Waziri
Ummy alipongeza uongozi wa Wilaya ya Ubungo kwa kutambua umuhimu wa
kutekeleza kwa vitendo maelekezo ya serikali ya kuwatambua Wazee katika
Halmashauri na kuwapatia vitambulisho vitakavyo wawezesha kupata Huduma
za matibabu bila vikwao.
Alisema
kuwa Wazee ni asilimia 5.6 ya wananchi wote wa Tanzania idadi ambayo
kwa kiasi kikubwa inaleta msukumo wa nchi kuweka mifumo madhubuti ya
kuhudumia Wazee ikiwemo kurahisisha upatikanaji wa Huduma katika
matibabu.
Alisema
kuwa Jambo hilo ni kuzingatia ukweli kwamba Wazee wanakabiliwa na
changamoto mbalimbali zinazosababishwa na umri mkubwa na mtazamo wa
Jamii ambao umekuwa ukichangia ukiukwaji wa haki na maslahi ya Wazee
katika ngazi mbalimbali.
Alisema
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imeingia kwenye rekodi kwa kuwatambua
Wazee wasio na uwezo kwani watapatiwa vitambulisho vitakavyo wawezesha
kupata Huduma za matibabu Bure.
Mhe
Ummy alisema kuwa Halmashauri zingine kote nchini zinapaswa kuanzisha
haraka zoezi la kuwathamini Wazee kwa kuwapatia Huduma Bora za afya
kabla ya kutoa Huduma za matibabu kwa Wazee kote nchini kwa kuanzisha
dirisha maalumu na wataalamu wa kuwahudumia Wazee.
Alitoa
Rai kwa watoa Huduma wa Afya kuviheshimu vitambulisho wakati wote Wazee
wanapoenda navyo kupatiwa matibabu huku akiwasihi Wazee kutumia
vitambulisho hivyo kwa kuzingatia maelekezo sio kwa kuwapa watu wengine
wasiohusika navyo.
Aidha
waziri Ummy ameahidi bima ya afya kwa watoto 100 wenye umri chini ya
miaka 18 wanaoishi kwenye mazingira magumu wilaya ya Ubungo na
uandikishwaji utaanza leo pia ameahidi kujenga wodi ya wazazi, watoto na
maabara ya damu kwenye kituo kimoja cha afya wilaya ya ubungo mara
baada ya kusikia hotuba ya kaimu mganga mkuu wa wilaya ya Ubungo.
Muheshimiwa
waziri ameiomba jamii kujiunga na bima za afya za gharama nafuu ili
kupunguza mzigo kwa halmashauri na kulinda afya za wananchi
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori alisema kuwa
lengo la uzinduzi huo wa ugawaji wa vitambulisho ni kuonesha umma kuwa
Wilaya ya Ubungo inawajali Wazee ikiwa ni Sehemu ya utekelezaji wa ilani
ya ushindi ya Chama Cha Mapinduzi katika kipindi Cha mwaka 2015-2020,
sera ya Taifa ya Wazee ya mwaka 2003 na sera ya Afya ya Mwaka 2007.
Mhe
Makori alisema kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Uongozi wa
Mheshimiwa Dkt John Pombe Magufuli imejipanga kuhakikisha Wazee wote
nchini wanapata Huduma Bora za afya bila vikwao hivyo Wilaya ya Ubungo
imeanza na utoaji vitambulisho kea Wazee 7296 waliojiandikisha na zoezi
hilo litakuwa endelevu.
Naye
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizungumza na
mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com mara baada ya uzinduzi wa ugawaji
wa vitambulisho vya Tiba kwa Wazee alisema kuwa Manispaa ya Ubungo
imetekeleza agizo la serikali lililotolewa na Waziri Mkuu kwenye
maadhimisho ya siku ya Wazee Octoba 1, 2009 kuwa Hospitali zote na Vituo
vya Afya vya Umma kutenga dirisha na watumishi maalumu wa Afya kwa
ajili ya kutoa Huduma za matibabu bure kwa Wazee.
Mkurugenzi
Kayombo alisema kuwa Manispaa ya Ubungo ina jumla ya Vituo 19 vya
kutolea Huduma za afya ikiwa ni pamoja na Hospitali moja, Vituo vya afya
vitatu, Zahanati 15, na Kliniki Moja ya Mama na Mtoto hivyo Vituo hivyo
vyote vitaanza kutoa Huduma za matibabu kwa Wazee wasio na uwezo bila
malipo.
vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure kwa Wazee katika
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam.
Kalli
amepongeza uongozi wa serikali Wilaya ya Ubungo kwa kutekeleza ilani ya
CCM ya ushindi yenye mkataba na wananchi kwa kipindi cha miaka mitano
2015-2020
SHARE
No comments:
Post a Comment