VIONGOZI wa Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma wameishukuru
serikali kwa kukarabati sekondari ya Mpwapwa ambayo majengo yake yalikuwa yana
hali mbaya.
Viongozi hao wametoa shukrani hiyo mbele ya Naibu Waziri Ofisi
ya Rais, Tamisemi Mhe. Selemani Jafo alipokuwa katika ziara ya kikazi kukagua
ukarabati wa shule hiyo.
Shule hiyo ni miongoni mwa shule 88 kongwe zinazokarabatiwa na
serikali ambapo katika awamu ya kwanza ukarabati umeanza kwa shule 43.
Katika shule hiyo, Serikali imefanikiwa kujenga bweni moja jipya
la wasichana, ukarabati wa mabweni 12 ya wavulana, ukarabati wa vyumba vya
madarasa 22, bwalo la chakuka pamoja na jiko, maktaba, maabara tatu, ofisi za
walimu, mfumo wa maji na umeme ambapo jumla ya sh.bilioni 1.2 zimetumika.
Akizungumza na viongozi katika ziara yake,Naibu Waziri Jafo
ameipongeza Kamati ya ujenzi kwa kufanyakazi bila kuchoka na kufanikisha
kuibadili kabisa shule hiyo ambayo kwasasa imegeuka kuwa shule bora ya kisasa
tofauti na ilivyokuwa awali.
Naibu Waziri Jafo amewataka wanafunzi wa shule hiyo kusoma kwa
bidii kwani serikali ya Dk. John Magufuli imeamua kuboresha miundombinu pamoja
na vifaa vya kutolea elimu kwa lengo la kufanikisha elimu bora hapa nchini.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua
majengo yaliyo karabatiwa na serikali katika sekondari ya Mpwapwa, Mkoani
Dodoma.
Baadhi ya madarasa ya
Mpwapwa sekondari yaliyo karabatiwa.
SHARE
No comments:
Post a Comment