
Watanzania wakishangilia na
kucheza katika JAMAFEST aliyevaa safari suti ni Naibu Balozi wa
Tanzania nchini Uganda Bw. Elibariki Maleko.

Aliyesimama na kushika Microphon
Bw. Iddi Suwed Mkurugenzi Mkuu wa Kikundi cha taifa cha tarabu cha
Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar wakati
wakitumbuiza nchini Uganda.

Wasanii wa kikundi cha Taifa cha Wizara Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar wakicheza ngoma ya asali ya Zanzibar.

Aliyevaa suti ya bluu na skafu ya
bendendera ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanania ni Kaimu Balozi ambaye
pia ni Naibu Balozi wa Tanzania Nchini Uganda Bw. Elibariki Maleko,
aliyevaa shati jeupe ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni,
Utalii na Michezo wa Tanzania Bara Profesa Elisante Ole Gabriel wa Naibu
Katibu Mkuu wake Bi. Nuru Milao wakiangalia ngoma za utamaduni katika
unoesho la usiku.

Baadhi ya Watanzania wakiangalia ngoma za utamaduni wakati wa onesho la sanaa usiku

Wasanii wa kikundi cha Kakau Band kutoka Bukoba wakitumbuiza katika jukwaa la Tanzania wakati wa mchana.

Wasanii wa kikundi cha Taifa cha
Utamaduni cha Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar
wakicheza ngoma ya Msewe ambayo ni maafuru Kisiwani Pemba.
……………………
KAMPALA
Tamasha la Sanaa na Tamaduni
la Jumuiya ya Afrika Mashariki JAMAFEST limeanza rasmi jana katikati ya
mji wa Kampala kwa wasanii wa sanaa za ubunifu za ngoma za utamaduni
kwa kuoneshwa bidhaa zao mbali mbali za Nchi Wanachama wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki.
Katika jukwaa la Tanzania
Kikundi cha Taifa cha Utamaduni cha Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni
na Michezo cha Zanzibar, Jinogile Band, Kakau Band na kikundi cha
Taarabu cha Taifa cha Zanzibar vilitia fora na kuwa kivutio kikubwa kwa
wananchi waliofika katika Tamasha hilo.
Tamasha la Utamaduni na Sanaa
la Jumuiya ya Afrika Mashariki linatarajiwa kufunguliwa rami leo na Rais
wa Uganda Kaguta Yoweri Museveni katika viwanja vya Kololo na kauli
mbiu ya Tanasha hili ni Utamaduni na ubunifu wa viwanda ni injini ya
umoja na ajira
JAMAFEST ni tamasha lenye
lengo la kuwaunganisha wasanii wasanaa za ubunifu za utamaduni kwa
kutafuta soko la bidhaa hiyo adimu yenye wazalishaji wengi katika nchi
za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo inakuza sekta ya utalii katika
Jumuiya na kwa mwaka huu Tanzania imewakilishwa na washiriki zaidi ya
200.
Washiriki wa Tanzania katika
maonesho ya jana kwa upande wa Tanzania yaliongozwa na Kaimu Balozi
ambaye pia ni Naibu Balozi wa Tanzania Nchini Uganda Bw. Elibariki
Maleko, Mshauri wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
wa Mambo ya Utamaduni na Utalii Mhe. Chimbeni Kheri, Katibu Mkuu wa
Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa Tanzania Bara Profesa
Elisante Ole Gabriel wa Naibu Katibu Mkuu wake Bi. Nuru Milao pamoja na
Watanzana wanaoishi na kusoma nchini Uganda.
Washiriki wa Tanzania wamekuwa
na lengo la kuonesha bidhaa ngoma za utamaduni, nguo, shanga, dawa za
mitishamba, lugha ya kiswahili, vyakula, mapishi na ulimbwende.
Habari na Picha
Wizara ya Mambo y Nje n Ushirikiano wa Afrika Mashariki
SHARE
No comments:
Post a Comment