TRA

TRA

Wednesday, September 13, 2017

Vitendo vya Ukatili kwa Watoto vyapungua Ilala

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

 

HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilala imesema vitendo vya ukatili  wanavyofanyiwa watoto chini ya miaka 18 vimepungua  kutoka kesi 199 zilizoripotiwa kwenye vituo vya polisi kwa mwaka 2016 hadi kesi  109 ziliropitiwa kwenye vituo hivyo kwa mwaka 2017.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Ofisa Mkuu wa Idara ya Jamii na Ustawi wa Jamii na Vijana wa Manispa hiyo Francisca Makole akitoa taarifa ya mwaka ya maendeleo ya ukatili katika halmashauri ya wilaya ya Ilala,  amesema vitendo hivyo vimepungua kutokana na elimu wanayotoa kwa jamii.

Amesema kutokana na elimu hiyo kumekuwa na ushirikiano unaotolewa na jamii hususani katika kuripoti matukikio hayo ya ukatili kwa watoto kwenye mamlaka husika. Alibainisha pia ukatili wa kingono umepungua kutoka   asilimia 32 kwa mwaka jana hadi kufikia asilimia 19 kwa  mwaka huu.

 “Sahivi watu wamekuwa mstari wa mbele kutoa taarifa pindi mtu anapofanyiwa ukatili wowote katika jamii,hususani kutoa taarifa kwenye kituo cha  mkono kwa mkono ambacho kinatumika kutoa huduma ya kupinga ukatili wa kijinsia,hii imechangia kupungua kwa vitendo vya ukatili’’ amesema Makole.

Makale amesema kwa sasa wamekuwa wakishirikiana na watu mbali mbali ambao wanajitolea kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ili kuweza kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia ndani ya manispaa hiyo.

Mratibu  wa kituo cha kupokea malalamiko ya watu wanaofanyiwa vitendo vya kijinsia cha One stop center , Sufian Mrisho amesema licha ya jamii kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa mapema pindi wanavyofanyiwa vitendo hivyo lakini bado jamii imekuwa ikipoteza ushahidi wa kuwati hatiani wanaofanya vitendo vya ukatili.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger