Vikosi vya usalama
nchini Togo vimerusha gesi ya kutoa machozi mapema leo, kutawanya mamia
ya waandamaji wanaoipinga seikali walioshinda usiku kucha mjini Lome.
Waandamanaji walikesha mitaani kupinga utawala wa Gnassingbe Togo
Vyombo vya habari vimekuwa vikichapisha picha za waandamanaji wakilala barabarani usiku.Polisi walichukua hatua ya maandamano ya nchi nzima ya saa 48 ya kutaka kumalizika kwa utawala wa miaka 50 wa familia ya Gnassingbe
Maandamano yaliendelea licha ya Rais Faure Gnassingbe, kuahidi kurejesha sheria ya kutaka rais ahudumu kwa mihula miwili pekee nchini humo.
Mamlaka zimeamrisha kuzimwa kwa mitandao kwa muda wa siku mbili kama njia ya kukabiliana na maandamano hayo.
CHANZO: BBC
SHARE









No comments:
Post a Comment