TRA

TRA

Tuesday, September 12, 2017

Wabunge kuondoa umri wa kuwania urais Uganda

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !




Wabunge kutoka chama kinachotawala nchini Uganda NRM wamekubaliana kuwasilisha mswada ambao unapendekeza kuondolewa miaka ya kuwania urais nchini Uganda.

Ikiwa watafaulu mswada huo utamwezesha Rais Yoweri Museveni ambaye anaaminika kuwa mwenye umri wa miaka 73, kuwania tena uchaguzi wa mwaka 2021.

Amekuwa madarakani tangu mwaka 1986 na kwa sasa anahudumu muhula wake wa tano madarakani.
Mswada ambao huo amabo unaungwa mkono na wabunge 200 wa NRM unataka kukifanyia mabadiliko kipengee cha 102 (b) cha katiba ya Uganda, ambacho kinaweka umri ambao mtu anaweza kuwania urais wa kati ya miaka 35 na 75.

Wengi wanasema kuwa NRM ambacho kina wabunge wengi, kitasababisha mabadiliko ya katiba lakini wengine ndani ya NRM wamekana.Wabunge wanasema kuwa watawasilisha mswada huo bungeni katika kipindi cha wiki moja.

CHANZO: BBC

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger