
Meneja
vipaji wa TBL Group na ABINBEV kanda ya Afrika Mashariki,Lilian Makau
(kulia) akiwa na baadhi ya wanafunzi waliochaguliwa katika awamu ya
kwanza ya mchujo wa kuingia mafunzo ya utawala wa kibiashara ya ABINBEV.(Kushoto) ni Meneja wa Programu hiyo ya mafunzo, Eth Baise.

Wanafunzi walioingia kinyanganyiro cha awamu ya kwanza wakijieleza

Wanafunzi walioingia kinyanganyiro cha awamu ya kwanza wakijieleza



Baadhi ya wanafunzi waliochaguliwa wakisikiliza maelezo wakati wa usahili.

Afisa Masuala Endelevu wa TBL Group,Irene Mutiganzi akitoa ufafanuzi wakati wa usahili huo

Baadhi ya wanafunzi wasichana waliofuzu kuingia mchujo wa awamu ya kwanza wakiwa kwenye chumba cha usahili

Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Group na ABINBEV wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa vyuo vikuu walioshiriki kwenye usahili.
………………………………………………………………
Awamu ya kwanza ya mchakato
wa kuwapata wanafunzi wa vyuo vikuu walioomba kujiunga na mafunzo ya
kimataifa ya uongozi wa kibiashara (Global Management Training Program)
ambayo yalizinduliwa hivi karibuni nchini na kampuni mama ya TBL Group
ya ABINBEV nchini unaendelea ambapo katika awamu ya kwanza wanafunzi 14
kutoka vyuo vikuu mbalimbali wamefuzu kuingia katika mchujo wa awamu ya
kwanza na usahili kwa wanafunzi hao ulifanyika mwishoni mwa wiki katika hoteli ya SeaCliff jijini Dar es Salaam.
Akiongea juu ya program hiyo,Mkurugenzi wa masuala ya sheria na masuala ya nje wa TBL na ABINBEV kanda ya Afrika Mashariki,Georgia Mutagahywa,alisema kuwa inafurahisha kuona maelfu ya vijana wamejitokeza kuomba kuingia
kwenye program hiyo japo nafasi sio nyingi ambapo baada ya kuyapitia
maombi wamechaguliwa wanafunzi 14 na mchakato wa kuwafanyia usahili
unaendelea ili kupata 3 watakaoungana
na wenzao kutoka nchi mbalimbali za Afrika kupata mafunzo hayo ya
kuwaandaa kuwa viongozi wa biashara na viwanda baada ya miaka michache
ijayo.
“TBL
na ABINBEV tunafurahi kuona vijana wa kitanzania wanapata fursa hii ya
kuwapatia utaalamu wa kuongoza biashara na uendeshaji wa shughuli za
viwanda kwa ufanisi hususani katika kipindi hiki ambacho Tanzania ina
mkakati mkubwa wa kuimarisha sekta ya viwanda nchini.Programu hii ni
endelevu tuna imani itawanufaisha vijana wengi wa kitanzania”Alisema Mutagahywa.
Kwa upande wake,Meneja wa Kuendeleza vipaji wa ABINBEV kanda ya Afrika,Rene Kohler-Thomas,alisema kuwa mafunzo haya yameishaonyesha mafanikio makubwa katika nchi ambazo kampuni hiyo inaendesha biashara zake na sasa ndio yamezinduliwa rasmi barani Afrika.
Alisema
katika kipindi cha awamu ya kwanza ya mafunzo haya zimechaguliwa nchi
za Afrika ya Kusini,Tanzania,Kenya na Nigeria na lengo kubwa ni kuwanoa
vijana wahitimu wasio na uzoefu wa kazi kupata elimu na uzoefu na
wakishahitimu kupatiwa fursa za uongozi wa ngazi za juu katika biashara za kampuni zilizopo kwenye nchi mbalimbali.
“Ndoto
yetu kubwa kama kampuni ni kuwaleta watu pamoja katika ulimwengu
maridhawa (Better World) katika kutimiza ndoto hii na kuhakikisha bidhaa
zetu zinaingia katika masoko mapya moja ya mkakati wake ni kuvutia
wateja wapya na kuondoa mipaka na ndio maana tunatoa fursa kwa wote
kujiunga na kufanya kazi na sisi”.Alisema Rene Kohler-Thomas
Alisissitiza
kuwa hii ni fursa pekee kwa vijana wa kitanzania watakaochaguliwa
kujiunga na program hii inayojulikana kama Global Management Training
Programme kwa kuwa watapata ujuzi wa fani mbalimbali sambamba kupata
mafunzo ya vitendo kwenye kampuni zilizopo chini ya ABINBEV sehemu
mbalimbali duniani.
Rene Kohler-Thomas alisema kwa watakaofanikiwa kujiunga
watapata mafunzo kwa muda wa miezi 10 mfululizo ambapo wanapata mafunzo
ya nadharia na vitendo ndani na nje ya kampuni kwenye nchi mbalimbali
na kukutanishwa na kuzungumza na wataalamu waliobobea katika fani
mbalimbali za uendeshaji wa biashara na utawala.
“Wahitimu
walengwa zaidi katika program hii ni waliohitimu katika fani za
Biashara,Uchumi,Masoko,Uhasibu na fedha,Uhandisi na IT na fani
nyinginezo wenye vipaji kwa kuwa kampuni yetu inaamini katika kuwekeza
katika viongozi wa baadaye na ndio maana tumekuja na mpango wa kuwaandaa”.Alisema.
Mmoja
wa wanafunzi waliofuzu kuingia kinyanganyiro cha awamu ya kwanza, Ajra
Omary,kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi,akiongea kwa niaba ya
wenzake alipongeza jitihada hizi na kuongeza kusema kuwa uwekezaji
unaolenga kuleta manufaa kwa jamii ndio unaotakiwa kwa kuwa unafungua
milango ya ajira kwa watanzania na kuwapatia fursa za uongozi wazawa baada ya kupatiwa mafunzo ya kitaalamu hususani katika kipindi hiki kuelekea Tanzania ya viwanda
SHARE
No comments:
Post a Comment