
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa(Mb) akisalimiana na Kamishna
Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa alipofanya ziara ya kikazi ya
kukagua maandalizi ya kufufua Kiwanda cha Sukari na Kilimo cha miwa
katika Gereza la Mbigiri Mkoani Morogoro Septemba 2, 2017. Jeshi la
Magereza kwa kushirikiana na Mifuko ya Jamii ya PPF na NSSF limeingia
ubia katika mradi huo wa uchumi wa viwanda chini ya Kampuni ya MKULAZI.
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt Steven
Kebwe na kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa kwenda katika kijiji cha
Maseyu kufuatilia utendaji wa kampuni ya Zhong Fenq kama inafuata
sheria, kanuni na taratibu za nchi.
Waziri
Mkuu ametoa agizo hilo Septemba 2, 2017 wakati
akizungumza na viongozi na watumishi wa kiwanda cha Philp Morris
kinachotengeneza sigara aina ya Marlboro akiwa katika ziara yake ya
kukagua maendeleo ya viwanda mkoani Morogoro.
Agizo
hilo limefuatia malalamiko ya mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki
Mheshimiwa Omary Mgumba kuwa wawekezaji hao kutoka China wanaendesha
shughuli za uchimbaji wa mabo katika kijiji cha Maseyu wilayani Morogoro
bila ya kuwa na kibali.
Mheshimiwa
mgumba amesema tangu mwaka 2011 wawekezaji hao wameendesha shughuli zao
bila kulipa kodi za Serikali na tozo za Halmashauri, hivyo kuikosesha
Serikali mapato.
“Mheshimiwa
Waziri Mkuu katika kijiji cha Maseyu kuna Wachina wa kampini ya Zhong
Fenq wanachimba mabo na hawana kibali na hakuna kodi yoyote wanayolipa
Serikalini tangu mwaka 2010 walipoanza uzalishaji.”
Mbunge
huyo ambaye machimbo hayo yako jimboni kwake aliongeza kwamba licha ya
uongozi wa mkoa kwenda katika eneo hilo na kuizuia kampuni kuendelea na
uchimbaji hadi itakapopata vibali walikaidi na kuendelea na shughuli.
Waziri
Mkuu amesema hakuna muwekezaji anayeruhusiwa kufanya kazi bila ya
kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi. Hivyo ameagiza kesho Mkuu wa
Mkoa afuatilie Wachina hao na kuona namna gani wamezingatia sheria za
nchi.
Amesema
iwapo watabaini kwamba wawekezaji hao hawajafuata sheria, kanuni na
taratibu hatua zichukuliwe dhidi yao ikiwa ni pamoja na kuwaondoa katika
eneo hilo chini ya ulinzi na kuwasiliana na ubalozi wa China Nchini.
Pia
Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa watu wote wenye nia ya
kutaka kuwekeza katika miradi mbalimbali nchini Tanzania kuhakikisha
wanafuata sheria, kanuni na taratibu za uwekezaji.
Katika hatua nyingine Waziri
Mkuu amesema ni faraja kuona kiwanda cha Philp Morris kikiwa
kimekamilika tayari kwa kuanza uzalishaji wa sigara aina ya Marlboro
hivyo kuwezesha wakulima wa tumbaku nchini kuwa na soko la uhakika.
Amesema
miaka ya nyuma uzalishaji wa tumbaku ulipungua nchini kutokana na
wakulima kukata taama baada ya kukosa soko la uhakika pamoja na
kuchoshwa na ubadhilifu wa mali za ushirika uliokuwa ukifanywa na
viongozi wa vyama vya ushirika wa tumbaku.
Pia
Waziri Mkuu alitembelea ujenzi wa kiwanda cha sukari kilichopo katika
Gereza la Mbigiri wilayani Kilosa na kukagua shamba la miwa lenye ukubwa
wa hekta 4,800 ambapo hekta 320 zimelimwa na kati yake hekta 125 tayari
zimepandwa miwa na imeshaota.
Kiwanda
hicho kinajengwa kwa ushirikiano wa Jeshi la Magereza na mifuko ya
hifadhi ya Jamii ya NSSF na PPF kupitia mradi wa Mkulazi ambao
unatarajia kuzalisha tani 250,000 za sukari kwa mwaka kati yake tani
50,000 zitazalishwa katika kiwanda cha Mbigiri na tani 200,000 katika
kiwanda cha Ngerengere.
Amesema
uwepo wa viwanda nchini utawezesha watanzania kulima kilimo chenye tija
kwa kuwa watauza mazao yao viwandani na mmoja atashiriki kulima zao
ambalo ataliuza katika kiwanda cha jirani.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa(Mb) akiangalia mbegu za miwa
kabla ya kuzipanda katika eneo la Shamba la miwa alipowasili Gereza
Mbigiri katika ziara ya kikazi ya kukagua maandalizi ya kufufua Kiwanda
cha Sukari na Kilimo cha miwa katika Gereza la Mbigiri Mkoani Morogoro
Septemba 2, 2017. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,
Bunge, Ajira na Watu wenye ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama.

Shamba la miwa katika mradi wa
Kiwanda cha Sukari na Kilimo cha miwa – MKULAZI katika eneo la Gereza la
Mbigiri Mkoani Morogoro likiwa limestawi kama inavyoonekana katika
picha.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akitoa hotuba fupi kwa
Maafisa na askari wa Jeshi la Magereza Mkoani Morogoro, Watendaji wa
Kampuni ya MKULAZI pamoja na Wananchi wanaoishi jirani na Gereza Mbigiri
katika ziara ya kikazi ya kukagua maandalizi ya kufufua Kiwanda cha
Sukari na Kilimo cha miwa katika Gereza la Mbigiri Mkoani Morogoro
Septemba 2, 2017.

Kamishna Jenerali wa Magereza,
Dkt. Juma Malewa akitoa maelezo mafupi kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim(hayupo pichani) namna Jeshi hilo
lilivyojipanga katika kuhakikisha kuwa ufufuaji wa Kiwanda cha Sukari na
Kilimo cha miwa katika Gereza la Mbigiri Mkoani Morogoro unakamilika
kama ilivyopangwa ambapo matarijio ni kuwa Kiwanda hicho kitakuwa na
uwezo wa kuzalisha sukari tani 50,000 kwa mwaka.

Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa
Jeshi la Magereza pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wa
Mkoani Morogoro wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua
maandalizi ya kufufua Kiwanda cha Sukari na Kilimo cha miwa katika
Gereza la Mbigiri Mkoani Morogoro Septemba 2, 2017.

Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof.
Godius Kyaharara akitoa maelezo mafupi kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa alipofanya ziara ya kikazi ya
kukagua maandalizi ya kufufua Kiwanda cha Sukari na Kilimo cha miwa
katika Gereza la Mbigiri Mkoani Morogoro Septemba 2, 2017.

Kamishna Jenerali wa Magereza,
Dkt. Juma Malewa(kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Viwanda, Biashara
na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage(kulia) mara baada ya ziara ya Waziri
Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ambapo amekagua maandalizi ya kufufua Kiwanda
cha Sukari na Kilimo cha miwa katika Gereza la Mbigiri Mkoani Morogoro
Septemba 2, 2017.

Mkurugenzi Mkuu wa PPF William
Erio akitoa neno la shukurani mbele ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa alipofanya ziara ya kikazi ya
kukagua maandalizi ya kufufua Kiwanda cha Sukari na Kilimo cha miwa
katika Gereza la Mbigiri Mkoani Morogoro Septemba 2, 2017.

Ujenzi wa maghala ya kuhifadhia
sukari katika mradi wa Kiwanda cha Sukari cha MKULAZI kilichopo Gereza
Mbigiri ukiendelea katika hatua mbalimbali kama inavyoonekana katika
picha

Wataalam wazalendo ambao
wanajitolea katika ujenzi wa mradi wa Kiwanda cha Sukari – MKULAZI
Mbigiri wakitambulishwa mbele ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim
Majaliwa(hayupo pichani(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Maafisa Waandamizi wa PPF na NSSF wakifuatilia kwa makini hotuba ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa(hayupo pichani).
SHARE
No comments:
Post a Comment