
Kesi mbili zimewasilishwa katika
mahakama ya juu nchini Kenya, zikitaka kufutwa kwa ushindi wa rais Uhuru
Kenyatta kufuatia uchaguzi wa tarehe 26 mwezi Oktoba.
Kesi hizo ziliwasilisha mahakamani Jumatatu saa chache kabala ya siku ya mwisho.
Aliyekuwa mbunge wa kilome Harun
Mwau na mawakili Njonjo Mue na Khelef Khalifa, wanasema kuwa katiba
ilikiukwa wakati wa maandalizi ya uchaguzi huo.
Kesi ya mwau ambayo inawashtaki
IEBC, mwenyekiti wake na Rais Uhuru Kenyatta ambaye alitangazwa mshindi
kwenye uchaguzi wa mwezi Oktoba, inasema kuwa kushindwa kwa IEBC
kuruhusu vyama kuandaa uchaguzi wa vyama, kuliwanyima wale ambao
walitaka kugombea fursa ya kufaya hivyo.
Mwau alijumuisha kipengee cha
uamuzi wa mahakama, kuwa mgombea kwa chama cha United Democratic Cyrus
Jirongo alikuwa amefilisika kwa hivyo hakustahili kuwania urais.
Kesi iliyowasilishwa na mawakili
Mue na Khalifa nayo kwa upande mwngine ilizunguzia ukiukaji wa katiba
ikiwemo kuchapisha picha za watu wasiostahili kwenye makaratasi ya urais
akiwemo mgombea wa muungano wa NASA Raila Odinga, ambaye alikuwa
ametangaza kuwa hangegombea urais.
Akiongea na vyombo vya habari
wakati wa kuandika kesi hiyo, wakili wa Mue na Khalifa, Harun Ndubi,
alisema kwa tume ya uchaguzi haukustahili kuandaa uchaguzi kwa hivyo
wanataka uchaguzi huo kuandaliwa upya.
Ndubi alisema kuwa tume ya uchaguzi ilikuwa na upendeleo kwa hivyo haikustahili kuandaa uchaguzi.
Ndubi aliwaambia waandishi wa
habari kuwa kumjumuisha Odinga kwenye makaratasi ya kura licha ya yeye
kujiondoa kuliwachanganya wapiga kura.
CHANZO:BBC SWAHILI
SHARE
No comments:
Post a Comment