NAHODHA wa timu ya taifa ya
Tanzania ‘Taifa Stars’ anayekipiga na KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana
Samatta atakuwa nje ya uwanja kwa majuma sita akiuguza majera ya goti
aliyopata katika mchezo wa ligi kuu uliomalizika kwa sare tasa dhidi ya
Lokeren.
Samatta alishindwa kuendelea
na mchezo baada kuumia dakika ya 40 nafasi yake ikachukuliwa na Nikos
Karelis aliyerejea hivi karibuni baada ya kukaa nje kwa muda mrefu pia
kutokana na majeraha.
Ripoti ya daktari
iliyotokana na majibu ya vipimo alivyofanyiwa straika huyo jana inasema
amepata jeraha dogo katika misuli ya goti inayofahamika kitaalamu kama
‘Literal Ligament’ huku pia maungio ya mfupa wa paja na wa ugoko
(meniscus) yakionekana kuathirika pia.


“Literal ligament imechanika
kidogo, hiyo itapona yenyewe lakini pia wamegundua tatizo kwenye
meniscus ambalo inabidi lifanyiwe upasuaji mdogo ili lisije kuleta shida
hapo baadae,” alisema Samatta
Upasuaji huo mdogo
utamlazimisha Samatta kukaa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki sita
akipata tiba na mazoezi huku timu yake ikiwa nafasi ya 10 kwenye msimamo
wa ligi kuu nchini Ubelgiji baada ya kukusanya pointi 19 pekee.
Samatta ndiye mshambuliaji
tegemeo klabuni hapo akiwa amejihakikishia nafasi ya kudumu kwenye
kikosi cha kwanza licha ya kuwepo kwa wakali kadhaa.
By Boiplus Media.
SHARE
No comments:
Post a Comment