Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
ameliagiza jeshi la Polisi nchini, kuendelea kuwapa kipaumbele askari wa
kike katika mafunzo mbalimbali ili waweze kukabiliana na vitendo vya
uhalifu mpya ambao umeanza kushika hatamu ukiwemo ugaidi, uchochezi,
uhafidhina, wizi wa mitandao na matumizi mabaya ya mitandao,
utakatishaji wa fedha haramu, ujangili, usafirishaji wa dawa za kulevya
na makosa mengine yanayovuka mipaka.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amesema hayo jana jijini Dar es
Salaam, alipokuwa akifunga maadhimisho ya miaka 10 ya Mtandao wa Polisi
Wanawake Tanzania(TPF NET) katika viwanja vya chuo cha Polisi Kurasini
yaliyokuwa na kauli mbiu ‘Usalama Wetu ni Mtaji wa Maendeleo, Tokomeza
Uhalifu Kuwezesha Uchumi wa Viwanda”.
“Tumeona juhudi zenu kwa kudhibiti uhalifu katika maeneo yaliyokuwa
korofi, ila ni jukumu lenu pia kuhakikisha kuwa mnakabiliana na vitendo
hivyo vya uhalifu,kuhakikisha havivurugi hali ya amani na kuhatarisha
usalama wa nchi”amesema .
Ameweka wazi kuwa ni wazi kwamba shughuli za kiuchumi zitafanyika
kikamilifu iwapo nchi itakuwa tulivu na yenye amani na kwamba amani na
utulivu huo,ndiyo utaleta kuaminiana na kukubaliana miongoni mwa
wananchi na wawekezaji, hivyo suala la ulinzi na usalama ni muhimu
katika maendeleo na ustawi wa nchi.
Alisema pamoja na kwamba jeshi hilo limejenga madawati ya jinsia ili
kukabiliana na tatizo hilo lakini kuna umuhimu wa kuzidisha utoaji wa
elimu kwa jamii ili kuwaelewesha kuwa wasiwe waoga wala wasione aibu
kuripoti matukio hayo.
Hata hivyo alisema, Serikali inajitahidi kuboresha jeshi la polisi kwa
kuendelea kulipatia vitendea kazi na itazidi kufanya hivyo kulingana na
bajeti iliyopo sambamba na kushirikiana na wadau wenye nia njema ya
kuwasaidia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akikagua gwaride maalum la polisi wanawake kwenye kilele cha
Maadhimisho ya miaka kumi ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania
yalioyofanyika kwenye Chuo Cha Taaluma ya Polisi,Kurasini, Dar es
Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akipata maelezo juu ya umuhimu wa alama za barabarani kutoka kwa
Koplo Faustina Nduguru wa Kitengo cha Usalama Barabarani makamo makuu ya
polisi Dar es Salaam wakati wa kilele cha Maadhimisho ya miaka kumi ya
Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania yalioyofanyika kwenye Chuo Cha
Taaluma ya Polisi,Kurasini, Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa
Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akipata maelezo juu kamera kugundua wanaoendesha kwa mwendo mkali
kutoka kwa Konstabo Sharifa Ismail wa Kitengo cha Usalama Barabarani
makamo makuu ya polisi Dar es Salaam wakati wa kilele cha Maadhimisho ya
miaka kumi ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania yalioyofanyika kwenye
Chuo Cha Taaluma ya Polisi,Kurasini, Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya
Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akizungumza na Kamishna wa Polisi Jamii Mussa Ali Mussa ambaye
alimkaimu Mkuu wa Jeshi la Polisi kwenye kilele cha Maadhimisho ya
miaka kumi ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania yalioyofanyika kwenye
Chuo Cha Taaluma ya Polisi,Kurasini, Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya
Makamu wa Rais)
SHARE
















No comments:
Post a Comment