
“Ofisi yangu ina jukumu
la kutoa taarifa sahihi na kwa wakati ya Serikali; Kusajili na kufungua
Magazeti; Kusaidia Watu wa mifumo mingine ya Serikali kusema” – Dk. H.A
@TZ_MsemajiMkuu
“Uhuru wa vyombo vya
habari upo wa kutosha. Serikali imeruhusu uhuru wa Vyombo vya habari.
Kuna Redio zaidi ya 150, tuna redio zaidi ya 30, kuna Magazeti zaidi ya
110 yanayotoka nchini” – Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
“Serikali ina simamia
Wananchi wapate habari sahihi na si kulishwa habari mbovu. Serikali
tunalisimamia hili” – Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
“Changamoto iliyopo ni kuhakikisha habari zsahihi zinawafikia Watu wote kwa wakati” – Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
“Rais @MagufuliJP
amefanikiwa sana kuleta mageuzi ya kifikra. Kujenga hari ya Uzalendo,
nidhamu, uwajibikaji kwa Watu wake wakiwemo Watumishi wa Umma na
Wananchi” – Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
“Rais @MagufuliJP
ameleta nidhamu kubwa ya matumizi ya fedha za umma. Mathalani
amefanikiwa kudhibiti safari za nje zisizo na tija” – Dk. H.A
@TZ_MsemajiMkuu
“Hapo nyuma zilitumika
bilioni zaidi ya 200 kwa safari tu wakati hivi sasa zimetumika bilioni
25 tu kwa safari tumeokoa pesa nyingi”@TZ_MsemajiMkuu
“Rais @MagufuliJP
ameleta mageuzi ya kudhibiti Wafanyakazi hewa zaidi ya 20,000 na kuokoa
zaidi ya Tsh. Bilioni 238. Ni mageuzi makubwa” – Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
“Tumeondoa wafanyakazi hewa takribani elfu 20 kwa zoezi hilo tumeokoa bilioni 238” @TZ_MsemajiMkuu
“Hawa wanaopiga kelele
juu ya mageuzi ya rasilimali za madini. Ipo siku watanyamaza wakiona
manufaa ya wazi. Serikali ya @MagufuliJP imeonyesha uzalendo kwenye
madini” – Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
“Zipo nchi kubwa duniani awapati 50/50 kwenye Madini sisi tumeweza @TZ_MsemajiMkuu
“Serikali itaendelea kuhakikisha kila kilicho chetu tunakipata”@TZ_MsemajiMkuu
“Kwenye vyeti feki
Serikali ya Rais @MagufuliJP imeokoa zaidi ya Tsh. Bilioni 148 ambazo
zinaenda kwenye shughuli za kimaendeleo.” – Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
“Sekta ya habari ni
sekta nyeti na Sheria hii ya habari tuliyo nayo sasa imeleta maboresho
na ubora kwenye sekta ya habari nchini” – Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
“Huwezi kutoa habari kwa kuingilia faragha ya mtu” @TZ_MsemajiMkuu
“Huwezi ukakiacha kituo cha radio kinawachochea wakulima wakawaue wafugaji arafu ukasema wana haki ya habari “@TZ_MsemajiMkuu
“Sheria mpya ya huduma
ya habari vimeweka ustawi wa vyombo vya habari na si kweli ipo kwa ajili
ya kufungia habari.” – Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
“Popote duniani hakuna nchi yenye sheria inayosema andika chochote” @TZ_MsemajiMkuu
“Hakuna nchi yeyote
Duniani inayotoa Uhuru kwa vyombo vyao vya habari kuwa na uhuru wa
kuandika chochote kile wanachojisikia” – Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
“Uandishi wa habari ni taaluma sasa ukikiuka sisi kama serikali hatuwezi kukuacha”@TZ_MsemajiMkuu
“Sisi tunailea sekta yote ya habari”@TZ_MsemajiMkuu
“Wananchi wapuuze habari kuwa Serikali inafungia vyombo vya
habari inapojisikia bali ina zingatia sheria” – Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
“Chombo cha habari kinatakiwa kifuate miiko”@TZ_MsemajiMkuu
“Vijana waamue kufanya
kazi, wawe Wazalendo, wamwogope Mungu. Safari ya Mabadiliko ni ngumu
lakini inahitaji uvumilivu” – Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
“Watanzania wamuunge mkono Rais @MagufuliJP atimize utekelezaji wa ilani ya uchaguzi” – Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
“Mwakani 2018 mwezi
Julai Serikali italeta ndege kubwa ya kisasa itakayokuwa inakwenda
popote pale Duniani” – Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
Mheshimiwa Rais
@MagufuliJP alikuta mikopo inatolewa kiasi cha bilioni 48 kwa mwaka
Lakini sasa hivi tumefikia bilioni 472 @TZ_MsemajiMkuu
“Fedha zipo na watapata kila mwanafunzi mwenye haki ya kupata”@TZ_MsemajiMkuu
“Serikali ya Rais
@MagufuliJP inatoa Tsh. Bilioni zaidi ya 400 kwa Wanafunzi. Kwa mara ya
kwanza fedha imetangulia vyuoni kabla ya Wanafunzi kuanza masomo” – Dk.
H.A @TZ_MsemajiMkuu
“Serikali imeboresha makusanyo kutoka Tsh. Trilioni 9.9 mpaka Tsh. Trilioni 14 kwa mwaka” – Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
Mheshimiwa @MagufuliJP
alipoingia madarakani tulikuwa tunakusanya kodi kwa kiasi cha “Trilioni
9.9.Leo hii tunakusanya trilioni 14 kwa mwaka haya ni mafanikio
makubwa”@TZ_MsemajiMkuu
“Serikali imeleta miradi
ya kihistoria nchini ya kuzalisha umeme kupitia miradi ya Kinyerezi 1
& 2” – Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
“Hivi tunapozungumza kuna watu hawalali kuna watu wanajenga reli Usiku na mchana”@TZ_MsemajiMkuu
Dk. Hassan Abbas ni
Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari na Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali
aliyasema hayo katika kipindi cha VijanaTz kilichorushwa Mubashara siku
ya Ijumaa Novemba 10, 2017 kupitia mitandao ya kijamii ya UVCCM ya
Twitter, Facebook na Instagram
IMEANDALIWA NA;
Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi
UVCCM Taifa
SHARE








No comments:
Post a Comment