
Spika wa bunge la Catalonia, Carme Forcadell, aliwasili katika Mahakama Kuu ya Madrid tarehe 9 Novemba 2017.
Spika wa bunge la Catalonia, Carme Forcadell, amelipa Euro 150,000
kama dhamana, ambayo itamruhusu aondoke gerezani kuanzia Ijumaa hii,
msemaji wa Mahakama Kuu amesema. Carme Forcadell alitakiwa kulipa dhamana hiyo kama sharti la kuachiliwa huru.
"Dhamana ya Forcadell imepokelewa, bado
kuna kusa agizo la majaji la kumuachilia huru," msemaji wa Mahakama Kuu
amewaambia waandishi wa habari. Bibi Forcadell anafuatiliwa katika
uchunguzi wa kuanzisha"uasi" na "uchochezi" uliozuka baada ya tangazo la
uhuru lililotolewa na bunge la Catalonia Oktoba 27.Spika wa bunge la
Catalonia, Carme Forcadell, mwenye umri wa miaka 58, na wabunge wengine
watano walisikilizwa siku ya Alhamisi na jaji wa Mahakama Kuu ya Madrid,
Pablo Llarena.
Wanatuhumiwa kufuata "mkakati wa pamoja
wa kutangaza uhuru," kabla ya tamko rasmi la bunge la Catalonia tarehe
27 Oktoba, tamko lililofutiliwa mbali siku ya Jumatano na Mahakama ya
Katiba. Mzozo huu mbaya unaoendelea nchini Uhispania haujawahi kutokea
tangu kuanza kwa mfumo wa demokrasia nchini humo miaka 40 iliopita.
Kiongozi wa Catalonia aliyetimuliwa
Carles Puigdemont na mawaziri wake wanne wako uhamishoni nchini
Ubelgiji. Mapema wiki hii walisikilizwa na mahakama ya Ubelgiji, na kish
wakaachiwa huru. Waziri Mkuu wa Ubelgiji Charles Michel alisema
katikati ya juma hili kuwa masuala ya Uhispania hayawezi kushughulikia
nchini Ubelgiji.
Chanzo:RFI
SHARE








No comments:
Post a Comment