
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL wakifuatilia hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh.Samia Suluhu Hassan

Baadhi ya wafanyakazi wa TBL katika matembezi ya AMREF ya kuchangisha fedha za kusomesha wauguzi fani ya ukunga

Baadhi ya wafanyakazi wa TBL wakifuatilia hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh.Samia Suluhu Hassan
………………………………………………………………..
Kampuni ya TBL Group imeshiriki kudhamini matembezi ya kuchangisha fedha za kusomesha wauguzi wakunga yaliyoandaliwa na Shirika
lisilo la kiserikali la AMREF yaliyofanyika jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki na kuongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania,Mh.Samia Suluhu Hasan,ambapo pia baadhi ya wafanyakazi
walishiriki katika matembezi hayo.
Akiongea
baada ya kumalizika matembezi hayo juu ya kampuni kushiriki,Meneja
Mawasiliano wa TBL,Zena Tenga,alisema kampuni inao mkakati wa kusaidia
na kushirikiana na wadau mbalimbali wanaofanya jitihada za kuunga mkono
zitihada za serikali katika kupambana na changamoto mbalimbali za
kijamii.
“Tunawapongeza AMREF kwa kuona umuhimu wa kulivalia njuga suala la kusomesha wauguzi fani ya ukunga kwa kuwa kwa kiasi kikubwa tukiwa na wakunga wa kutosha wenye utaalamu kutaaidia kupunguza idadi ya vifo vya wanawake wajawazito na watoto wachanga wakati wa kujifungua.
Tenga alisema kuwa TBL itaendelea kuunga mkono jitihada hizi kama ambavyo imeamua kuvalia njuga changamoto nyingine za kijamii hususani katika kuboresha sekta za elimu na afya nchini.
SHARE








No comments:
Post a Comment