Kampuni kinara ya simu za mkononi TECNO imeungana na Vodacom kutambulisha toleo jipya TECNO Phantom 8, Simu hiyo iliyozinduliwa nchini Dubai imetambulishwa rasmi nchini Tanzania katika duka la TECNO SMART HUB lililopo Mlimani City mapema mwezi huu.

Akizungumza wakati wa utambulisho ,
Afisa mahusiano wa TECNO , Eric Mkomoya amesema ‘’ TECNO
tumeitambulisha rasmi Phantom 8 nchini Tanzania leo tukiwa na mshirika
wetu wa matoleo ya Phantom nchini , Vodacom .Tumetengeneza simu bora
yenye hadhi, tunayofuraha kuwataarifu wateja wetu kuwa Phantom 8
inapatikana katika Smart Hubs za TECNO na maduka yote ya Vodacom
nchini.’’ Alihitimisha
Akizungumza na waandishi wa
habari Mkuu kitengo cha mahusiano Vodacom Jackline amesema ‘’ TECNO
inataraji wateja wake kufurahia matumizi ya toleo jipya la simu janja
iliyopo sokoni ambayo tayari imejipatia umaarufu kwa kupokelewa vizuri
sehemu mbali mbali nchini Tanzania .Vodacom inawazawadia meseji 300 ,
5GB za kuperuzi mtandaoni , na dakika 300 za kupiga mitandao yote kwa
wateja watakao nunua Phantom 8 katika maduka ya Vodacom yaliyopo
nchini kote .
Phantom 8 ina 6GB RAM,Betri yake
ina uimara wa 3500 mAh za kuhifadhi chaji kwa muda mrefu, 64 GB ROM,
inayoipa simu uwezo wa ziada wa kuhifadhi data kufikia 2TB , Inavuta
picha iliyombali kwa ukaribu bila kupoteza muonekano halisi mara 10
zaidi ya simu za kawaida . Phantom 8 ina muundo na mtindo wa kuvutia
hasa rangi yake yenye mng’ao wa almasi

Ushirikiano baina ya TECNO na
Vodacom umekua wa kudumu ambapo awali waliitambulisha Phantom 6 na 6+
sasa wanakuletea Phantom 8 inayotikisa soko ikiwa na 20MP kamera ya
mbele na 12MP +13 MP kamera zake 2 za nyuma.

Mwandishi wa habari Asia Matona alijinyakulia zawadi ya Phantom 8 kwa hisani ya TECNO na Vodacom.
Kwa maelezo zaidi kuhusiana na TECNO tafadhali tembelea tovuti yetu ya http//www.tecno-mobile.com
SHARE








No comments:
Post a Comment