Mkurugenzi wa Uchumi wa Benki Kuu
ya Tanzania (BoT), Bw. Johnson Nyella
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
BENKI
Kuu ya Tanzania BoT, inakusudia kufanya mabadiliko ya mfumo wa kuandaa Sera ya
Fedha (Monetary policy) ifikapo Machi 2018, Mkurugenzi wa Uchumi wa Benki Kuu
ya Tanzania (BoT), Bw. Johnson Nyella, amewaambia
waandishi wa habari wanaoshiriki semina ya siku tano ya habari za Uchumi,
Biashara na Fedha mkoani Mtwara.
Kwa sasa BoT
inatekeleza Sera ya Fedha kwa kulenga wingi (quantity) wa shilingi au kwa
maneno mengine (ujazi wa fedha) ili ziwe na uwiano muafaka na vitu halisi,
alisema mtaalamu huyo nguli wa uchumi wa BoT.
“Mfumo huu
tunaotarajia kuuanza utakuwa unaangalia riba kama kiashiria cha mafanikio ya
Sera ya Fedha na riba yenyewe itakuwa inaamuliwa na riba ya sera yaani
policy rate.” Alibainisha,
Bw. Nyella
alisema, riba ya sera itakuwa inaamuliwa na kamati ya Sera ya Fedha au
Monetary Policy Committee na ikishaamuliwa BoT itachukua hatua mbalimbali za
kisera kuhakikisha kwamba riba iliyoko katika soko la mabenki la kukopeshana
inalingana au inakuwa karibu kabisa na ile riba ya sera au policy rate na ndio
utaratibu utakaotumika.” Alifafanua.
Mfumo ambao
unatumia wingi (quantity) wa fedha, tatizo lake ni kwamba kama kukiwa na
mabadiliko ya utashi wa shilingi katika
uchumi, mfumo huo utakuwa unaendelea kuweka ukwasi wa kiwango kile kile cha, malengo
ya mwanzo yaliyokuwa yamewekwa, na inaweza kutokea wakati huo shilingi
haihitajiki lakini kulikuwa na malengo makubwa ya kuweka shilingi katika uchumi
na hivyo kupelekea kuyumba kwa bei katika uchumi, alisema.
“Mnapokuwa
mmeweka malengo ya bei au ya riba maana yake
ni kwamba hata kukitokea mabadiliko ya utashi, demand ya shilingi
ikipungua mtekeleza sera utaona kwamba riba inaongezeka na hivyo benki
itachukua hatua ya kupunguza shilingi kwenye uchumi .” Alisema.
Kinyume chake
hitajio (demand) la fedha likiongezeka mtekeleza sera atachukua
hatua ya kuongeza shilingi kwenye uchumi ili ziendane na mabadiliko ya utashi
(hitajio) la fedha
“Kwa hiyo
mfumo unaotumia bei unaubora zaidi kwa vile unauwezo wa kwenda na mabadiliko ya
utashi (demand) wa fedha wakati mfumo unaotumia ujazi wa fedha
(quantity) unakosoro na hauwezi kwenda na mabadiliko ya utashi yanayaotokea
katika uchumi kwa haraka kiasi cha kutosha.” Alifafanua Bw. Nyella.
Alisema mfumo
huo mpya ndio unaotumika kwa sasa na benki nyingi duniani na maamuzi ya kwenda
kwenye mfumo huo ni sehemu ya utaratibu ambao BoT umejiwekea wa kuboresha Sera
ya Fedha kila wakati lakini pia ni sehemu ya makubaliano na nchi za Jumuiya
ya Afrika Mashariki (EAC) ya kurazinisha ku harmonize Sera za Fedha katika Jumuiya.
Meneja
Msaidizi-Idara ya Uhusoano wa Umma na Itifaki, Benki Kuu ya Tanzania,
(BoT), Bi. Vicky Msina, (kushoto), akizunhguzma jambo akiwa
na Mkurugenzi wa Uchumi wa Benki Kuu
ya Tanzania (BoT), Bw. Johnson Nyella
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo.
Meneja wa BoT, tawi la Mtwara, Bw. Mussa
Mziya,(aliyekaa), akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa BoT, tawi la
Mtwara, Bw.Lucas Mwimo, (wapili kulia) na Meneja Msaidizi-Idara ya Uhusoano wa Umma na Itifaki, Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), Bi. Vicky Msina
Dkt. Suleiman Missango, Meneja
Msaidizi-Idara ya Utafiti, Kurugenzi ya Sera za Uchumi na Utafiti, BoT,
akifafanua baadhi ya masuala ya kiutendaji yaliyokuwa yakitolewa na
watoa mada kwenye warsha hiyo.
Mkurugenzi wa BoT tawi la Benki Kuu Mtwara, Bw.Lucas Mwimo akitoammada kuhusu nafasi ya matawi ya BoT, katika utekeelzaji wa majukumu ya benki hiyo.
Meneja wa BoT tawi la Mtwara Bw.Mussa Mziya akizungumza wakati wa semina ya waandishi wa habari za Uchumi, Biashara na Fedha.
|
Mtaalamu wa masuala ya mikopo ya nyumba
kutoka Benki Kuu ya Tanzania, Bw.Baraka D. Munisi, akitoa mada kuhusu
dhamana ya mikopo ya nyumba (Mortgage Finance)
SHARE
No comments:
Post a Comment