Mganga
Mkuu wa Serikali Profesa Mohammed Bakari (katikati) akikata utepe
kuashiria kupokea msaada wa vitanda 27 na magodoro yake kwa ajili ya
watoto wenye ulemavu wa vichwa na mgongo wazi,vilivyotolewa na Kampuni
ya mafuta ya Dalbit Tanzania,hafla hiyo ilifanyika katika wodi ya watoto
hao katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.Wengine
katika picha Mkurugenzi Mkuu wa Dalbit Tanzania,Margaret Mbaka(kulia)
na Mkurugenzi wa huduma za wauguzi wa Hospitali hiyo Flora Kimaro.
Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya mafuta ya Dalbit Tanzania,Margaret Mbaka( kulia)
akimfafanulia jambo Mganga Mkuu wa Serikali Prof.Mohammad Bakari juu
ya msaada wa vitanda 27 na magodoro yake kwa ajili ya watoto wenye
ulemavu wa vichwa na mgongo wazi,vilivyotolewa na Kampuni hiyo wakati wa
hafla ya kukabidhiwa msaada huo iliyofanyika katika Hospitali ya Taifa
ya Muhimbili jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa huduma
za wauguzi wa Hospitali hiyo Flora Kimaro.
Ofisa
Uhusiano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Patrick Mvungi na Mkuu wa
kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni ya mafuta ya Dalbit
Tanzania, Anthony Kagiri,wakibandika stika kwenye vitanda na vifaa
mbalimbali vilivyotolewa msaada na kampuni hiyo kwa ajili ya watoto
wenye ulemavu wa vichwa vikubwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
vyenye thamani ya shilingi Milioni16/-
SHARE
No comments:
Post a Comment