Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb), mwenye tai ambaye ndiye alikuwa Mgeni Rasmi
katika hafla ya uzinduzi wa kitabu cha Dkt. Salim Ahmed Salim (Salim
Ahmed Salim: Son of Afica), kitabu kinachozungumzia historia iliyotukuka
ya Dkt. Salim ndani ya Tanzania, Afrika na Duniani kwa ujumla, wakiwa
wameshikilia kitabu hicho baada ya kuzinduliwa rasmi tarehe 21-01-2016,
katika hafla iliyofanyika katika hoteli ya New Africa jijini Dar es
Salaam.
Waziri Mahiga akikata utepe, kama ishara ya kuzindua kitabu hicho.
Mhariri wa kitabu hicho, Dkt. Jackkie Cilliers akizungumza katika hafla hiyo.
Waziri
wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa,
Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb), ambaye ndiye alikuwa Mgeni Rasmi
katika hafla ya uzinduzi wa kitabu cha Dkt. Salim Ahmed Salim (Salim
Ahmed Salim: Son of Afica),akimzungumzia historia iliyotukuka ya Dkt.
Salim Ahmed Salim, kabla ya uzinduzi wa kitabu hicho.
Dkt.
Salim Ahmed Salim, akitoa maneno ya Shukrani kwa heshima aliyopewa kwa
Mwandishi wa kitabu hicho lakini kwa wadau wote waliohudhuria hafla hiyo
ya uzinduzi wa kitabu chake. Aliyekua Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula (Katikati), akiwa na wageni mbalimbali wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho.
Waziri Mahiga akifurahia jambo na Dkt. Salim.
Aliyekua Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe akisalimiana na baadhi ya wageni waliohudhuria hafla hiyo. Dkt. Salim akizungumza jambo wakati wa hafla hiyo. Mgeni Rasmi, Waziri Augustine Mahiga akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kuzindua kitabu cha Dkt. Salim katika hafla iliyofanyika tarehe 21-01-2016 katika hoteli ya New Africa jijini Dar es Salim. PICHA NA REUBEN MCHOME.
SHARE
No comments:
Post a Comment