Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Utalii,Bi. Uzeeli Kiangi akisisitiza jambo wakati
alipokuwa anamkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,
Meja. Generali. Gaudence Milanzi kufungua Mkutano Mkutano wa Kamati ya
Uwezeshaji Utalii ( Tourism Facilitation Committee- TFC) uliofanyika leo
Mpingo House jijini Dar es Salaam wa kujadili changamoto mbalimbali
zinazoikabili sekta ya Utalii nchini.
Katibu Mkuu
wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja. Generali. Gaudence Milanzi (
kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Utalii Bw. Deogratius Mdamu
(kushoto) wakimsikiliza Mjumbe ( hayupo pichani ) wakati wa Mkutano wa
Kamati ya Uwezeshaji Utalii ( Tourism Facilitation Committee- TFC)
uliofanyika leo Mpingo House jijini Dar es Salaam akiwa anazungumzia
changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Utalii nchini na kutoa
ushauri ya namna kuuimarisha Utalii wa ndani ambao umekuwa bado ni
changamoto kwa wananchi wengi kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo
nchini
Baadhi ya
Wajumbe wa kamati ya Uwezeshaji Utalii ( Tourism Facilitation
Committee- TFC) wakiwa wanajadili changamoto mbalimbali zinazoikabili
sekta ya Utalii nchini kwa kutoa maoni, ushauri na ufumbuzi wa
changamoto ikiwa na kuchangia mikakati mbalimbali itakayowezesha
kusaidia kuhamasisha Utalii wa ndani.
Wakati nchi
nyingi Afrika zikiwa zinafanya jitihada mbalimbali za kuimarisha Utalii
wa ndani ambao umekuwa ndo wa uhakika katika kuiingizia nchi mapato hata
pale majanga yanapotokea, Nayo Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na
Utalii imeendelea kuhakikisha kuwa Utalii wa ndani unakua kwa kasi
inayotarajiwa
Baadhi ya
Majanga hayo yanayoathiri Sekta ya Utalii ni milipuko ya magonjwa kama
Ebola, matukio ya Ugaidi Kenya na kushuka kwa Euro ya Ulaya dhidi ya
Dola ya Marekani.
Hivyo
Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Wadau wa Utalii nchini
wamepanga mikakati ya kuhakikisha kuwa Utalii wa ndani unakuwa tegemeo
tofauti na sasa ambapo Watalii kutoka nje ndio wamekuwa wamekuwa
wakitembelea hifadhi zetu kwa kiasi kikubwa.
Akizungumza
kwenye Mkutano wa Kamati ya Uwezeshaji Utalii ijulikanayo kama Tourism
Facilitation Committee ( TFC) uliofanyika leo Mpingo House jijini Dar
esSalaam , Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili, Meja. Generali. Gaudence
Milanzi na Utalii amesema maendeleo ya Utalii yanahitaji sana Utalii wa
ndani kuimarika baadala ya kudhani kuwa vivutio vya utalii vilivyopo ni
kwa ajili ya wageni kutoka nchi za nje.
Meja.
Generali. Milanzi amesema Utalii ni sekta nyeti sana katika kuliingiza
Taifa pesa za kigeni lakini hata hivyo ni sekta ambayo imekuwa
inaathirika kwa haraka sana pindi majanga yanapotokea nchi jirani hivyo
ni lazima jamii ijengewe utamaduni wa kutembelea vivutio vya Utalii ili
kuweza kujihakikishia Watalii wa ndani wanakuwa wengi.
Baadhi ya
mikakati iliyopendekezwa na Wajumbe wa kamati ya Uwezeshaji Utalii
(TFC) ni kuwawezesha maafisa Utalii wa Halmashauri wanatengewa bajeti ya
kutosha, wanajengewa uwezo kuhusu ya vivutio vya utalii vilivyopo
kwenye maeneo yao pamoja na Idara ya Utalii kufungua ofisi kila kanda
ili kuweza kutimiza majukumu yake ipasavyo.
Aidha,viwanja
vya ndege vilivyopo nchini viimarishwe ikiwa pamoja na nchi kuwa ndege
zake kama ilivyo kwa nchi jirani kama Kenya na Rwanda Awali , Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Utalii,Bi. Uzeeli Kiangi alisema Mkutano wa TFC
hutoa fursa za kuziibua na kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili
sekta ya Utalii hivyo Sekta Binafsi zinawajibu mkubwa wa kuhakikisha
changamoto zinazoikabili sekta zinatafutiwa ufumbuzi Aliongeza kuwa
Idara ya Utalii imekuwa ikishiriki katika maonesho mbalimbali ya kitaifa
lengo likiwa ni kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa kutembelea
vivutio vya Utalii nchini.
Aidha,
Prof Wineastor Anderson amesema sekta ya Utalii imekuwa inakua lakini si
kwa kiwango cha kuridhisha hivyo jitihada za kutangaza utalii ndani na
nje nchi upewe uzito unaostahili kwa kuiwezesha Bodi ya Taifa ya Utalii
inatengewa bajeti ya kutosha.
Wakati
huo huo, Mwenyekiti wa Shirikisho la vyama vya Utalii Tanzania ( TCT)
Bw. Richard Rugimbana, amesema Utalii wa ndani ili uweze kukua suala la
elimu linahitajika kutolewa ili kuweza kuibadilisha jamii ipende
kutembelea vivutio vya Utalii.
Naye
Kamanda wa Polisi Jk Ndaki anayeshghulikia dawati la Utalii ( Tourism
Police Unit) amewahakikishia usalama wao watalii wa ndani na nje ya nchi
kutembelea vivutio vya Utalii bila hofu yoyote kuwa Jeshi la Polisi
nchini lipo macho muda wote.
SHARE
No comments:
Post a Comment