Zuwena Senkondo wkikabidhi vifaa vya kujifungulia kwa mmoja wa wauguzi katika zahanati ya Mwingiro Wilayani Nyang’wale Mkoani
Geita
|
Na Dixon Busagaga wa Globu ya jamii
Kanda ya Kaskazini,aliyekuwa mkoani Geita.
Mgodi
wa Dhahabu wa Bulyanhulu umekabidhi seti nane za vifaa vya kutolea huduma kwa
akina mama wajawazito wanapojifungua, katika halmashauri ya wilaya ya Nyang’wale
Mkoani Geita vyenye thamani ya shilingi Milioni Tatu.
Akipokea
vifaa hivyo Mratibu wa Huduma ya Baba, Mama na Mtoto wa Halmashauri ya Nyang’wale
Mkoani Geita Bi Neema Mhoja amesema, “Tunaushukuru Mgodi wa Dhahabu wa
Bulyanhulu kwa kutupatia vifaa hivi muhimu kwa ajili ya kuokoa maisha ya mama
na mtoto kwani awali upungufu wa vifaa hivyo umesababisha Wauguzi Wakunga
katika zahanati wilayani humo kutoa huduma katika mazingira magumu.”
Naye
Meneja wa Mahusiano ya Jamii wa Mgodi wa Bulyanhulu Bwana Elias Kasitila
amesema, afya za akina mama ni nguzo ya msingi wa maendeleo katika jamii hivyo
Mgodi kwa kutumia utaratibu wa kusikiliza kero za wananchi mwaka huu ulipata
maombi ya vifaa hivyo kutoka kwa wananchi wa vijiji vya Iyenze na Mwasabuka
katika kata ya Mwingiro wilaya ya Nyang’wale mkoani Geita na umeitikia ombi kwa
kukabidhi vifaa hivyo kwa mratibu wa huduma za akina mama na watoto wa wilaya
ya Nyang’wale.
Wauguzi
katika zahanati ya kata Mwingiro wamekabidhiwa vifaa hivyo ili waweze kuvitumia
na kuvitunza kwa ajili ya matumizi kwenye zahanati hiyo inayohudumia wakazi
wapatao 12,000 wa kata ya Mwingiro.
Muuguzi Mkunga wa zahanati ya Mwingiro bwa Costantine
Matata Bahebe, na Pendo Ntabudyo, na Elizabeth Lameck amesema, “ Sasa itakuwa
rah asana ukipata mzazi maana vifaa vinatosha kwani kwa mwezi tunazalisha akina
mama kati ya 20 na 25 hivyo kwa vifaa hivi tufanya kazi katika mazingira ya
usafi, usalama na utulivu hata pale tutakapopata wazazi nane kwani kila mmoja
atakuwa na kifaa chake kuliko kumsubirisha mzazi wakati unapochemsha vifaa
baada ya kuvitumia.
SHARE
No comments:
Post a Comment