Mwenyekiti
wa Kikundi chaYetu Envorotec Group kinachojishughulisha na kufanya
usafi katika Mtaa wa Gongo la Mboto Manispaa ya Ilala, Ali Mwinyimkuu
(kulia), akishiriki kufanya usafi na wananchi Dar es Salaam jana, ikiwa
ni utaratibu waliojiwekea wa kufanya usafi kila baada ya wiki mbili ili
kuunga mkono kauli Rais Dk. John Magufuli ya kufanya usafi katika maeneo
tunayoishi na kufanyia shughuli zetu nchini.
Kazi ya usafi ikiendelea.
Mwenyekiti
wa Kikundi chaYetu Envorotec Group kinachojishughulisha na kufanya
usafi katika Mtaa wa Gongo la Mboto Manispaa ya Ilala, Ali Mwinyimkuu
Omari akiwaongoza wenzake kufanya usafi.
Hapa ni kazi tu tunaukataa uchafu.
Wanawake wakishiriki kufanya usafi eneo la relini.
Mwenyekiti
wa Mtaa huo, Bakari Shingo (Aliyevaa kaputura), akishiriki kufanya
usafi na wananchi wake Dar es Salaam jana, ikiwa ni utaratibu
waliojiwekea wa kufanya usafi kila baada ya wiki mbili ili kuunga mkono
kauli Rais Dk. John Magufuli ya kufanya usafi katika maeneo tunayoishi
na kufanyia shughuli zetu nchini.
Usafi ukiendelea.
Wasanii wa Kikundi cha Rock Star wa Mtaa huo nao walishiriki kufanya usafi.
Na Dotto Mwaibale
WANANCHI
wa Mtaa wa Gongolamboto Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam
wameendelea kumuunga mkono Rais John Magufuli kwa kufanya usafi katika
eneo hilo kwa wiki mara mbili ili kuyaweka mazingira yao katika hali ya
usafi.
Akizungumza
na waandishi wa habari waliotembelea mtaa huo Dar es Salaam jana
kujionea shughuli za usafi katika eneo Mwenyekiti wa mtaa huo Bakari
Shingo alisema lengo lao kubwa ni kuiunga mkono kauli ya Rais Magufuli
ya kufanya usafi ambapo wao wameamua kufanya usafi kwa wiki mara mbili.
Alisema
lakini wao walianza kufanya usafi katika eneo kabla ya rais kuanza
kuhimiza lakini kauli ya Magufuli ilichochea zaidi moto wa kufanya usafi
kwa wananchi wa eneo hilo.
Shingo
alisema katika mtaa wao kunavikundi ambavyo vinasaidia kufanya usafi
ambapo wamegawa maeneo na utaratibu huo umesaidia kuyaweka mazingira
katika hali ya usafi.
Mwenyekiti
wa Kikundi chaYetu Envorotec Group kinachojishughulisha na usafi katika
mtaa huo Ali Mwinyimkuu Omari alisema kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa
katika suala zima la usafi katika eneo hilo kutokana na utaratibu
waliojiwekea.
Alisema
wanamshukuru Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Issaya Mngulumi kwa
kujitoa kwake kuwapa gari la kusomba takataka kila wanapofanya usafi
hali ambayo inawapa moyo wananchi wa kufanya usafi hivyo kumungana mkono
Rais Dk. John Magufuli katika suala zima la usafi nchini.
SHARE
No comments:
Post a Comment