Wanajeshi wa Kenya waliouawa
Wanajeshi
wa Kenya nchini Somalia walionywa kuhusu shambulizi la kundi la
Alshabaab siku 45 kabla ya kundi hilo kuvamia mojawapo ya kambi zao
,jenerali moja wa Somalia amesema.
Kenya ilipewa ripoti ya Intelijensi kuhusu tishio la uvamizi huo ,jenerali Abas Ibrahim Guery aliiambia BBC.
Wapiganaji
hao wa kiislamu wanasema kuwa waliwaua zaidi ya wanajeshi 100 katika
shambulio hilo likiwa ni baya zaidi kuwahi kufanyika kwa jeshi la Kenya.
Mkesha wa kumbukumbu ya kuwanezi wanajeshi waliouawa nchini Somalia
Jeshi la Kenya bado halijatoa idadi ya wanajeshi waliouawa ama hata kujibu matamshi ya jenerali Gurey.
Rais wa
Kenya Uhuru Kenyatta amewatambelea baadhi ya wanajeshi waliojeruhiwa
katika hospitali ya Jeshi iliopo Nairobi kabla ya kuhudhuria hafla ya
kuwakumbuka wanajeshi hao.BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment