Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha.
Tume ya
Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imetangaza tarehe ya marudio ya uchaguzi
visiwani humo baada ya matokeo ya uchaguzi uliopita kufutwa.
Uchaguzi huo sasa utafanyika Jumapili Machi 20, 2016. Tangazo hilo limetolewa na mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha.
Bw. Jecha amesema tarehe hiyo iliamuliwa na tume baada ya mkutano hapo jana.
“Uchaguzi
huo utahusisha uchaguzi wa Rais, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na
Madiwani na hakutakuwa na uteuzi mpya wa wagombea wala mikutano ya
kampeni,” amesema Jecha.
“Wagombea wote walioteuliwa hapo awali wataendelea kuwa wagombea katika uchaguzi huu.”
Chama cha
Wananchi (CUF) kimekuwa kikipinga kurudiwa kwa uchaguzi. Chama hicho
mapema mwezi huu kilionya kwamba hatua hiyo inaweza kusababisha vurugu.
Viongozi wa chama hicho walisusia maadhimisho ya Siku ya Mapinduzi wiki iliyopita.
Chama
tawala, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilikuwa tayari kimewashauri wanachama
wake visiwani wajiandae kwa marudio ya uchaguzi, tangazo
lililoshutumiwa vikali na viongozi wa CUF.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment