Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
amefungua tawi la Benki ya Posta iliyopo mjini Songea, wakati akiwa
katika ziara mkoni Ruvuma inayotarajiwa kumalizika jumatano wiki hii.
Akizungumza na uongozi na
wafanyakazi wa Benki ya Posta pamoja na wateja waliohudhuria ufunguzi
wa tawi hilo uliofanyika nje ya benki hiyo hapo jana, Waziri Mkuu
amesema amefarijika kuona benki hiyo iliyokua imekumbwa na matatizo
sasa imezaliwa upya na kumpongeza Mkurugenzi wa Benki ya Posta nchini
Bwana. Sabasaba Mushindi kwa jitihada zake za kufufua benki hiyo.
Amesema, Benki hiyo inalenga
wananchi wenye vipato vya chini, SACOSS, Vyama Vya Ushirika na
wafanyabiashara wadogo wadogo , nakusisitiza kuwa wafanyabishahara na
wananchi wa Ruvuma wanaweza kukopa ili kukuza mitaji yao lakini waweze
kurudisha mikopo hiyo ili iwanufaishe na wengine.
Waziri Mkuu Majaliwa, pia
amefurahishwa na huduma ya mikopo kwa wasataafu inayotolewa na benki
hiyo, ambapo amesema amefarijika kuona wazee nao wana nafasi ya kukopa
kupitia benki ya posta.
Pia, ametumia fursa hiyo kutoa
wito wa kuwataka watanzania kuacha tabia ya kutembea na fedha nyingi
mifukoni kwani hukaribisha wizi na kusababisha matumizi yasiyo na
mpangilio.
“Watanzania tubadilike , ni muhimu sasa watanzania kubadilika tuhifadhi fedha zetu Benki” alisema Waziri Mkuu.
Kwa upande wake,Mtendaji Mkuu wa
Benki ya Posta nchini Bwana. Sabasaba Mushindi amempongeza Waziri Mkuu
na Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli kwa kuchaguliwa na wananchi na
namna ambavyo wameendelea kuingoza Serikali chini ya kauli mbiu ya HAPA
KAZI TU.
Bwana. Mushindi amesema benki ya
Posta ilianzishwa miaka 90 iliyopita ikiwa chini ya utawala wa
kikoloni, ina lengo la kuchochea utamaduni wa kujiwekea akiba kwa
watanzania, takwimu zikionesha watanzania wako nyuma katika kuweka
akiba.
Chini ya 10% ya mapato ndio
yanawekwa kama akiba, na 14% ya watanzania wanaohifadhi fedha benki, na
3% tu ya watanzania wana sifa na uwezo wa kukopa benki.
Aidha, amesema baada ya
kukabiliana na changamoto mbalimbali hivi sasa benki ya Posta
inaendelea kuimarika ambapo wamekua wakipata faida na baada ya
mahesabu kukamilika wanatarajia kupata hadi kiasi cha bilioni 12 kwa
mwaka 2015.
“Hadi sasa 70% ya matawi ya benki
yamefanyiwa ukarabati, kumekuwepo na huduma kama PPT popote, akaunti ya
michezo (Sports account) ambayo imesaidia vilabu mbalimbali kama Mbeya
City na Stand United ya Shinyanga, pia benki imetoa kiasi cha shilingi
milioni 150 kusaidia makundi mbalimbali ya kijamii ” alisema Bwana.
Mushindi
SHARE
No comments:
Post a Comment