Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy
Mwalimu (Mb.)akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa
Maendeleo ya Mtoto, mbele ya Ofisi za Dawati la Jinsia na Watoto la Mkoa
wa Ruvuma.
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu (Mb.) leo
ametembelea Dawati la Polisi la Jinsia na Watoto la Mkoa wa Ruvuma,
kwa lengo la kufuatilia hali ya Ulinzi na Ustawi wa Mtoto Mkoani humo.
Wakati
wa ziara hiyo Mhe. Ummy Mwalimu aliwapongeza Wadau mbalimbali wa
Maendeleo ya Mtoto Mkoani Ruvuma kwa Ushirikiano waliouonyesha hadi
kufanikisha Ujenzi wa Kituo hicho.
Alieleza
kuwa kwa Mkoa wa Ruvuma Wizara yake kwa kushirikiana na Wadau wa
Maendeleo ya Mtoto, itahakikisha inashughulikia kwa haraka tatizo la
Usafirishwaji wa watoto kwenda nchi za jirani kutumikishwa katika kazi
mbalimbali.
SHARE
No comments:
Post a Comment