TRA

TRA

Tuesday, February 9, 2016

Bunduki iliyotungua ndege iyakamatwa

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu Lazaro Mambosasa akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) bunduki aina ya Riffle Na 7209460 CAR Na 63229, iliyotumika kuangusha helikopta na kumuua rubani wake Rodgers Gower (37) raia wa Uingereza katika tukio lililotokea ndani ya pori la akiba Maswa wilayani Meatu mkoani Simiyu.  Siku chache baada ya kutokea tukio la majangili katika pori la akiba Maswa wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu, kuitungua ndege (helikopta) iliyokuwa doria na kuawa kwa rubani wake Rodgers Gower (37) watu 9 wamekamatwa kuhusika na tukio hilo. 

Katika watuhumiwa hao mmoja alikuwa akifanya kazi katika hifadhi ya Ngororo kitengo cha Interejensia, ambaye alitajwa kuwa mhusika Mkuu wa kufanikisha tukio hilo sambamba na kukamatwa mganga wa jadi. 

Akitoa taarifa mbele za waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa polisi Mkoani hapa Lazaro Mambosasa alisema kuwa kukamatwa kwa watuhumiwa hao kumetokana na jeshi hilo kwa kushirikiana na wananchi, pamoja na uongozi wa TANAPA. 

Kamanda Mambosasa alisema watuhumiwa wote walikamatwa na kukiri kuhusika na tukio hilo, huku akieleza kuwa msako mkubwa uliofanywa na jeshi hilo mara baada ya tukio kutokea chini ya Mkuu wa upelelezi Mkoa Jonathan Shana. 

Alisema katika msako huo baadhi ya watuhumiwa walibainika kuwa kiungo kikubwa kufanikisha tukio hilo kwa kutoa mbinu za uharifu, huku wakijihusisha na matukio ya ujangili kwa muda mrefu. 

Aliongeza kuwa baadhi yao walibainika kuwa waganga wa jadi, ambapo walikuwa wakitoa dawa kwa majangili za kuosha silaha, ikiwa pamoja kuosha na kusafisha mihili yao ili wasiwe kukamatwa. 

Mambosasa aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Shija Mjika (38), Njile Gonga (28) Mhazabe, Masasi Mandago (48) pamoja na Dotto Pangali (41) , ambao ndiyo waliohusika kutungua helkopta hiyo. (P.T)

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger